HAKUNA kitu kizuri kama ukiwa kwenye uhusiano, unaoonyesha dalili zote za mafanikio kwa maana ya maelewano, masikilizano, kuheshimiana lakini kubwa zaidi uliotawaliwa na amani na upendo.
Jambo la msingi watu wanapaswa kulifahamu ni kwamba, wengi wetu huharibu wenyewe uhusiano tulionao kutokana na matendo yetu. Lakini pamoja na hayo, zipo njia zinazoweza kusaidia kulinda uhusiano, usiingie dosari na kuvurugika, kukosa maelewano lakini baya zaidi kuvunjika.
Jambo la kwanza la msingi ili kuulinda uhusiano wako si kwa mwanamume au mwanamke, ni upendo. Kila aliye katika uhusiano ahakikishe anamuonyesha mwenza wake upendo wa dhati na si kusubiri yeye ndio aonyeshwe upendo.
Kumbuka kumuonyesha mtu upendo si lazima umwambie unampenda kila saa au kila dakika la hasha, unaweza kumuonyesha mwenza wako upendo kwa vitendo tu. Mfanyie mambo ambayo unajua fika yatamfurahisha na yatamuonyesha dhahiri namna unavyomjali na kumpenda.
Pamoja na hayo, jambo lingine linalochangia kulinda uhusiano wako, ni kuhakikisha una msiri na mambo yenu ya ndani. Wengi hapa huvuruga kwa kutoa kila kitu cha uhusiano wao hadharani. Hali hii kwa kweli ni mbaya na inaweza kuvunja uhusiano husika.
Si jambo la ajabu kukuta wenza wanatukanana hadharani na kudhalilishana au kusimulia kwa mashoga na marafiki kila kinachojiri ndani ya uhusiano huo. Kumbuka si kila mtu anafurahia uhusiano ulionao, hivyo
Nitumie maoni yako kwa kubonyeza hapo chini

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni