Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt. Agustine Mahiga akizungumza wakati wa mkutano baina ya wawakilishi kutoka Tanzania na Afrika Kusini kuhusu majadiliano ya awali ya mikataba na makubaliano ya ushirikiano baina ya Tanzania na Afrika Kusini yanayotarajiwa kutiwa saini kesho wakati wa Ziara ya Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini anayetarajiwa kuwasili leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Afrika Kusini Maite Nkoana – Mashabane
SERIKALI ya Jamhuri ya Afrika Kusini imekubali kuendelea kuwafudisha marubani wa Tanzania ikiwa ni sehemu moja wapo ya kukuza maendeleo ya sekta ya uchukuzi na usafiri wa anga pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Augustine Mahiga ameyabainisha hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu majadiliano ya awali yaliyofanyika kati ya nchi hizo mbili juu ya mikataba mbalimbali inayotegemewa kusainiwa Mei 11 mwaka huu.
Balozi Mahiga alisema kuwa katika majadiliano hayo wamejadili mikataba iliyowahi kusainiwa kwa kupima utekelezaji wake pamoja na kujadili mikataba mipya iliyojikita katika sekta mbalimbali za maendeleo zikiwemo za uchukuzi, nishati, elimu pamoja na mawasiliano.
“Katika sekta ya uchukuzi tumekubaliana kuboresha barabara, usafiri wa anga pamoja na reli hasa ya TAZARA, sisi tumenunua ndege na tunaendelea kununua zingine zitakazosafiri hadi Afrika ya Kusini hivyo nchi hiyo imekubali kuendelea kuwafundisha marubani wa Tanzania kuendesha na kukarabati ndege hizo,”alisema Balozi Mahiga.
Nitumie maoni yako Kupitia
Fb.com

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni