Huyo ni miongoni mwa wale wanakwenda kupumzika katika nyumba ya milele
R. I. P KWA WALIOPOTEZA wapendwa inasikitisha sana
R. I. P
Ajali Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ametoa neno na kusema amepatwa na uchungu na majonzi baada ya kuona majeneza ya watoto na walezi wao ambao walipata ajali ya basi huko Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Rais Magufuli amesema hayo kupitia ukurasa wake wa twitter na kuwataka Watanzania kuomboleza msiba huu kwa umoja huku tukiwaombea marehemu hao wapumzike mahali pema peponi.
"Nimepatwa na uchungu na majonzi makubwa ninapoyaona majeneza ya watoto na walezi wao waliopoteza maisha katika ajali ya basi huko Arusha, tumewapoteza mashujaa wetu katika elimu. Tuwaombee na tuendelee kuwa na subira, uvumilivu na ustahimilivu, tunapoomboleza vifo vya wapendwa wetu tuendelee kuwa wamoja. Mungu ibariki Tanzania" alisema Rais Magufuli
Mbali na hilo miili yote ya marehemu ambayo imeagwa leo katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha imesafirishwa na kuelekea sehemu mbalimbali za nchi kwa ajili ya ndugu kufanya maziko ya wapendwa wao hao.
HAKUNA kitu kizuri kama ukiwa kwenye uhusiano, unaoonyesha dalili zote za mafanikio kwa maana ya maelewano, masikilizano, kuheshimiana lakini kubwa zaidi uliotawaliwa na amani na upendo.
Jambo la msingi watu wanapaswa kulifahamu ni kwamba, wengi wetu huharibu wenyewe uhusiano tulionao kutokana na matendo yetu. Lakini pamoja na hayo, zipo njia zinazoweza kusaidia kulinda uhusiano, usiingie dosari na kuvurugika, kukosa maelewano lakini baya zaidi kuvunjika.
Jambo la kwanza la msingi ili kuulinda uhusiano wako si kwa mwanamume au mwanamke, ni upendo. Kila aliye katika uhusiano ahakikishe anamuonyesha mwenza wake upendo wa dhati na si kusubiri yeye ndio aonyeshwe upendo.
Kumbuka kumuonyesha mtu upendo si lazima umwambie unampenda kila saa au kila dakika la hasha, unaweza kumuonyesha mwenza wako upendo kwa vitendo tu. Mfanyie mambo ambayo unajua fika yatamfurahisha na yatamuonyesha dhahiri namna unavyomjali na kumpenda.
Pamoja na hayo, jambo lingine linalochangia kulinda uhusiano wako, ni kuhakikisha una msiri na mambo yenu ya ndani. Wengi hapa huvuruga kwa kutoa kila kitu cha uhusiano wao hadharani. Hali hii kwa kweli ni mbaya na inaweza kuvunja uhusiano husika.
Si jambo la ajabu kukuta wenza wanatukanana hadharani na kudhalilishana au kusimulia kwa mashoga na marafiki kila kinachojiri ndani ya uhusiano huo. Kumbuka si kila mtu anafurahia uhusiano ulionao, hivyo
Nitumie maoni yako kwa kubonyeza hapo chini
JIJI la Arusha na vitongoji vyake jana lilisimama kwa simanzi, majonzi na vilio kwa zaidi ya saa tano wakati wa ibada maalumu ya maziko ya kitaifa ya wanafunzi 33 wa darasa la saba, walimu wawili na dereva mmoja wa Shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Lucky Vincent ya jijini Arusha waliokufa kwa ajali ya gari Jumamosi asubuhi.
Hali ilikuwa mbaya pale miili 35 iliyokuwa ikitolewa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kupelekwa kwenye Uwanja wa Michezo wa Shehe Amri Abeid Kaluta ambako ibada hiyo ilifanyika ikiongozwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan. Maiti hizo zilikuwa katika magari maalumu matatu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yenye namba za usajili 5611JWTZ08 aina ya IVIECO, gari lingine la jeshi hilo aina ya Ashok Leyland lenye namba za usajili 9123JWTZ na gari la tatu ni la aina hiyo hiyo lenye namba za usajili 9121JWTZ.
Msafara wa magari hayo ulianza saa 2.10 asubuhi kutoka Hospitali ya Mount Meru, lakini uliingia Uwanja wa Sheikh Amri Abeid saa 5.15 asubuhi, saa tatu zaidi kutokana na umati wa watu kuangua vilio barabarani pindi maiti hizo zilipokuwa zikipita na wengine kuzuia magari hayo kupita bila ya kujitambua kuwa wanafanya makosa. Askari wa JWTZ kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Arusha ilibidi wafanye kazi ya ziada kuwaondoa watu hao barabarani waliokuwa wakigalagala kwa vilio na kuwasogeza ili maiti hizo zipite na kuelekea uwanjani ambako uwanja huo unaochukua watu zaidi ya 15,000, lakini ulijaa pengine maradufu ya uwezo wake.
Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ilibidi kufanya kazi ya ziada kuwaasa wananchi wa Arusha kuruhusu magari hayo ya jeshi kupitia na kusiweze kutokea majanga mengine yasiyokuwa na msingi. Hali ya vilio na majonzi ilizidi zaidi pale miili hiyo ilipoingia kwenye uwanja huo wa michezo saa 11.15 asubuhi na kufanya watu zaidi ya 155 wakubwa kwa wadogo wakiwemo wanafunzi, kuanguka kwa kuzirai baada ya kupatwa na mshituko walipoona maiti zikiwa katika majeneza zikiingia uwanjani hapo.
Kwa mujibu wa Chama cha Msalaba Mwekundu Mkoa wa Arusha, watu zaidi ya 200 walizirai katika ibada hiyo ya jana. Magari ya kubeba wagonjwa yalilazimika kufanya kazi ya ziada kubeba wagonjwa waliokuwa wakianguka uwanjani na kuwakimbiza Mount Meru kupata matibabu ya awali. Maiti hizo zilipofikishwa uwanjani, ziliteremshwa kwa ustadi mkubwa na askari wa JWTZ kwa kushirikiana na vijana wa Skauti na kupelekwa uwanjani sehemu ilipotengwa kwa ajili ya ibada ya kuaga wanafunzi, walimu na dereva huyo waliokufa katika ajali ya barabarani eneo la Rhotia Marera wilayani Karatu wakati basi lao aina ya Mitsubishi Rosa lilipotumbukia korongoni wakiwa safarini kwenda wilayani humo kwa mitihani ya ujirani mwema.
Hali ilizidi kuwa mbaya zaidi kwa wazazi wa wanafunzi waliokufa katika ajali hiyo kwani hawakuweza kujizuia na kila mmoja aliangua kilio pale alipoona jeneza la mtoto wake likiwa na msalaba na kuandikwa jina kamili. Hali hiyo ya kilio kwa kila mzazi ilisababisha hata viongozi mbalimbali wa serikali na vyama wakiongozwa na Makamu wa Rais, Samia waliokuwepo katika ibada hiyo maalumu, kuinamisha vichwa vyao kwa simanzi na wengine kujikaza kwa kufuta machozi kwa vitambaa vyao vya mikononi.
MAKAMU WA RAIS Akizungumza katika ibada hiyo maalumu, Makamu wa Rais, Samia amewataka madereva kote nchini kuwa waangalifu na makini wanapofanya kazi zao za kila siku kwani wajue kuwa wanabeba roho za watu. Alisema serikali kila siku imekuwa ikiwakumbusha madereva kuacha kutumia vilevi pindi wanapoendesha vyombo vya moto kwani kwa kufanya hivyo ni kutenda kosa kubwa sana, na aliwakumbusha madereva kuwa iwapo watakuwa makini na waangalifu katika kuendesha magari, ajali nyingi zinaweza kuepukika.
Mbali ya hilo, amewataka wamiliki wa magari na madereva kubeba abiria wanaostahili katika vyombo vyao vya usafiri kwa kufanya hivyo kunaweza kuepuka ajali. Alisema vifo vya wanafunzi, walimu na dereva wa shule hiyo ya awali na msingi yenye makao yake Kwamrombo jijini hapa, vimeleta huzuni kubwa sana kwa nchi na Rais John Magufuli ametoa salamu za kuwapa pole sana wafiwa na wakazi wote wa Jiji la Arusha kutokana na msiba huo mkubwa. Aliwashukuru watalii ambao ni madaktari bingwa kutoka Marekani kwa msaada mkubwa waliotoa ajali ilipotokea na kuwataka kuendeleza ukarimu huo sehemu yoyote bila ya kificho.
Alisema madaktari hao baada ya ajali ndio waliokuwa wa kwanza kufika katika eneo la tukio na kutoa huduma ya kwanza na hatimaye kufuatilia hadi hospitalini walikopelekwa, hiyo ni kiasi gani walitimiza wajibu wao wa upendo kwa nchi kwa kuwashughulikia majeruhi na wengine kupoteza masiha. Makamu wa Rais alimshukuru Rais Uhuru Kenyatta na wananchi wake wa Kenya kwa kushiriki kikamilifu katika msiba huo na pia kumtuma Waziri wa Elimu kushiriki ibada hiyo inatia moyo ni jinsi gani Kenya ilivyo karibu na Tanzania.
MBOWE Naye Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, alisema jana ilikuwa siku muhimu sana kila Mtanzania kutafakari amani ya kitaifa. Mbowe alisema Chadema na vyama vyote vya upinzani vitakuwa mstari wa mbele na Serikali Kuu na Mkoa katika kuhakikisha kila jambo la msingi linakwenda sawa na kuwapa pole wale wote waliofikwa na msiba huo.
Alisema msiba huu ni mkubwa na Watanzania wote. KINANA Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, kwa niaba ya wanachama wa chama hicho kote nchini na wabunge wake, alitoa pole nyingi sana kwa msiba huo na kuwataka wafiwa kuwa na uvumilivu katika kipindi hicho kigumu kwao. Kinana aliyeingia uwanjani hapo na Makamu wa Rais saa 3.40 asubuhi, alisema kila mtu aliyekuja uwanjani hapo ana dini na kifo ndicho huunganisha watu na kuacha tofauti zao na kuangalia kilicho mbele.
Alitumia muda mfupi sana kuongea na kuwataka wakazi wa Jiji la Arusha, wazazi na walimu kuwa wapole katika wakati huu. WAZIRI WA ELIMU KENYA Kabla ya kuingia kwa miili hiyo uwanjani, kulikuwa na salamu za viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Elimu wa Kenya, Fred Matiang’i, ambaye alisema ametumwa na Rais Uhuru, kuwa nchi yake imeguswa na msiba huo mkubwa. Matiang’i alisema wananchi wa Kenya wakiongozwa na Rais wao, wako bega kwa bega na Serikali ya Tanzania katika kuomboleza msiba huo na kuwapa pole wazazi, walezi na ndugu wa wanafunzi, walimu na dereva waliokufa katika ajali hiyo.
“Nimekuja hapa siku ya leo nimetumwa na Rais Uhuru kutoa pole na rambirambi za vifo hivyo na Kenya nzima imehuzunishwa sana, na Serikali ya Kenya imetoa pole sana kwa wale wote waliofiwa. Mungu aendelee kuwafariji na kuwapa pole katika kipindi hiki kigumu kwani sisi sote ni wamoja na katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na ni lazima tushirikiane kwa hali na mali katika kila jambo,” alieleza waziri huyo wa Elimu Kenya.
SALAMU ZA SMZ Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed, alisema kwa niaba ya Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Serikali ya Baraza la Mapinduzi wamesikitishwa na tukio hilo na wako katika majonzi na huzuni kubwa kwa msiba huo. Aboud alisema SMZ iko mstari wa mbele katika jambo hilo na kuwataka wazazi, walezi na ndugu kuwapa pole katika kipindi hiki kigumu na wao watatoa rambirambi ikiwa ni njia ya kuwafariji wafiwa.
MAWAZIRI WATOA NENO Vingozi wengine waliopata fursa ya kuzungumza ni baadhi ya mawaziri, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.
Pia walikuwapo viongozi wa dini, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa. Dk Mpango alisema alikuwa Arusha kushiriki kikao cha bajeti na mawaziri wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), lakini alipopata taarifa hiyo ilimsikitisha na hakutaka kuondoka na kusubiri ibada jana. Alisema watoto na wengine waliofariki katika ajali hiyo wanapaswa kupongezwa kwani wamefariki wakiwa kazini wakisaka elimu. Kwa upande wake, Profesa Ndalichako alisema wanafunzi na walimu wamekufa wakiwa katika harakati za kusaka elimu hivyo kazi ya Mungu haina makosa.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera, alisema kwa niaba ya wakuu wa mikoa yote na yeye kama jirani anawapa pole sana wazazi na wananchi wote wa Arusha. Bendera alisema msiba hauzoeleki na kila mtu ameguswa na msiba huo na kila mmoja wetu anawapenda sana wanafunzi na walimu wao, lakini Mungu amewapenda sana na ndio maana amewachukua ghafla.
KAIMU JAJII MKUU Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, aliwapa pole wale wote waliofiwa na kusema hiyo ilikuwa mipango ya Mungu. Jaji Juma alisema binadamu hupanga mipango yake, lakini Mungu naye hupanga mipango na kutekeleza na kuwataka wafiwa kuwa wapole katika kipindi hiki kigumu kwao. Alisema watoto hao walikuwa wakisaka mwanga wa elimu hivyo wanapaswa kuombewa kule waendako wapate mwanga zaidi.
MAENEO WANAKOZIKWA Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Gambo, wanafunzi waliopata ajali ya kufa wanasafirishwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwamo ya Nyanda za Juu Kusini katika Mkoa wa Iringa, Kyela mkoani Mbeya na Mkoa wa Tanga. Gambo alitaja maeneo mengine ya mbali ambayo yamegharamiwa na serikali ni mkoani Singida, Kondoa mkoani Dodoma, Rombo Mkoani Kilimanjaro na wanafunzi wengine wanazikwa jijini Arusha katika maeneo ambayo wafiwa watakuwa tayari kusema .
Pia baadhi ya miili ya watoto kadhaa imerudishwa hospitali walimokuwa wamepumzishwa wakisubiri siku ya kuzikwa jijini hapa; wengine wanazikwa leo, wengine kesho hadi Ijumaa katika maeneo tofauti. Gambo alisema gharama za majeneza, usafiri na nyingine zote zinagharamiwa na Serikali ya Mkoa wa Arusha na kuwataka wafiwa kushirikiana na kamati kwa kila jambo. SHULE YAFUNGWA Kwa mujibu wa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Lucky Vincent, Ephraim Jackson, shule hiyo imefungwa kwa wiki moja kwa sababu ya maombolezo ya msiba huo.
Nipe maoni yako kwa kubonyeza
===== NAZIRHAMZA
WATUHUMIWA nane vinara wa mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda mwaka 1994, bado wanasakwa kwa udi na uvumba na Umoja wa Mataifa ili wajibu tuhuma za ushiriki wao katika mauaji ya watu milioni moja nchini humo wengi wao wakiwa Watutsi.
Kati ya hao nane, watatu ambao ndio watuhumiwa wakuu watashtakiwa katika chombo kinachosimamia kazi zilizobaki za iliyokuwa Mahakama ya Mauaji Kimbari ya Rwanda (ICTR) ambayo imemaliza muda wake miaka miwili iliyopita.
Chombo hicho (MICT) kimepewa majukumu ya kuwatafuta, kuwakamata na kuwashtaki watuhumiwa watatu vinara wa mauaji hayo wakiongozwa na mfanyabiashara Felicien Kabuga ambaye anatajwa kuwa mmoja wa vinara wa mauaji hayo ya siku 100 nchini humo.
Ofisa Habari wa MICT,Danford Mpumillwa alisema mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa kazi ya kuwasaka watuhumiwa hao inaendelea kwa kushirikiana na serikali za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.
Aliwataja watuhumiwa wengine wawili vinara ambao wakikamatwa watafikishwa katika MICT mjini Arusha kuwa ni Augustin Bizimana ambaye alikuwa Waziri wa Ulinzi katika serikali ya Rais Juvenal Habyarimana na Protais Mpiranya aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha kumlinda Rais Habyerimana.
Watuhumiwa wengine watano, kwa mujibu wa Mpumillwa, wakikamatwa watapelekwa Rwanda kushtakiwa ambao ni Fulgence Kayishema, Charles Sikubwabo, Aloys Ndimbati, Pheneas Munyarugarama na mwingine aliyefahamika kwa jina moja tu la Ryandikayo.
“Nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa zinawajibika kuwakamata na kuwafikisha katika chombo hicho watuhumiwa hao na kikosi maalum cha kuwasaka kinaendelea kuwafuatilia katika nchi ambazo tunaamini wamejificha. Sasa ni wajibu wa serikali husika kushirikiana kuwakamata watuhumiwa ili wakajibu tuhuma dhidi yao na hii ni kazi ya kudumu,” alisisitiza Mpumillwa wakati wa mkutano wa pamoja wa majaji wa Chombo hicho, Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu (ACPHR), Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) na Mahakama Kuu ya Tanzania.
Akizungumza baada ya ufunguzi wa mkutano huo wa pili kufanyika Afrika, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma alisema kuwa una lenga kubadilishana uzoefu katika utoaji wa haki nchini.
“Tunajifunza kutoka kwa wenzetu namna bora na mazingira yatakayosaidia utoaji wa haki hapa nchini kwa kuzingatia uzoefu wa wenzetu na uwezo wa rasilimali walizonazo na hii itasaidia nasi kuiga yale yaliyo ndani ya uwezo wetu,” alisisitiza Profesa Juma.
MICT ni chombo kilichoundwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa baada ya ICTR kumaliza muda wake kusimamia kesi zilizobaki na kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka muhimu za kesi hizo zitakazotumiwa na wasomi kwa ajili ya utafiti wa kitaaluma kikiwa na makao makuu yake Lakilaki eneo la Kisongo jijini hapa.
Au maoni yako Kupitia
NazirHamza au

SIKU ya Mei 6 mwaka huu (2017) ni kati siku zitakazokumbukwa na wakazi Arusha na Tanzania kwa ujumla wake kwa muda mrefu.
Siku hii imeacha kumbukumbu mbaya kufuatia ajali mbaya ya gari iliyopoteza uhai wa wanafunzi 33 wa shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Lucky Vicent iliyopo eneo la Kwa Mrombo katika Jiji la Arusha.
Pamoja na wanafunzi hao 33 ambao wote ni wa darasa la saba pia katika ajali hiyo maisha ya walimu wawili wa shule hiyo, Innocent Pappian na Julius Mollel na dereva Dismas Kessy, walipoteza maisha hivyo kufanya idadi ya waliofariki katika ajali kufikia watu 36.
Walionusurika katika ajali hiyo ni wanafunzi wawili wa kike ambao hadi usiku wa kuamkia leo (Mei 7, 2017) walikuwa wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru ambao hata hivyo majina yao hayakuweza kupatikana mara moja.
Ajali hiyo mbaya ambayo itabaki katika kumbukumbu za ajali mbaya kuwahi kutokea mkoani Arusha na nchini ilitokea saa 2.30 asubuhi (Mei 6) katika kijiji cha Rhotia baada ya gari hilo kuacha barabara na kutumbukia katika korongo la mto Marera, lenye urefu unaokadiriwa kuwa kati ya mita 20 hadi 25.
Wanafunzi hao waliokuwa wakitumia usafiri wa basi la shule aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T 872 BYS walikuwa safarini kuelekea wilayani Karatu, kushiriki mitihani ya ujirani mwema na wenzao wa shule ya Tumaini Academy iliyopo mjini Karatu.
Basi hilo lilikuwa kati ya mabasi matatu ya shule hiyo yaliyokuwa yameongozana na taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa gari iliyopata ajali ilikuwa katikati.
Taarifa kutoka eneo la tukio na chanzo cha ajali
Bado hakuna uhakika wa taarifa rasmi kuhusu chanzo cha ajali hiyo lakini taarifa zilizopo zinadai kuwa ni kutokana na mfumo wa breki za gari hilo kushindwa kufanya kazi na hivyo dereva kushindwa kumudu usukani na gari kutumbukia korongoni.
Aidha taarifa nyingine zinadai kuwa dereva huyo alikuwa katika mwendo kasi eneo hilo ambalo lina mteremko mkali na kona kali hivyo kushindwa kuhimili mwendo kasi wa gari lake.
Lakini Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo aliwaambia waandishi wa habari kwamba polisi bado wanachungunza chanzo cha ajali hiyo na taarifa itatolewa kwa umma uchunguzi huo utakapokamilika.
Taarifa zilizopatika kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa wanafunzi 29 walifariki papo hapo pamoja na walimu wao wawili na dereva wa gari hilo na kufanya idadi ya waliokufa wakati huo kuwa 32.
Majeruhi walikimbizwa katika hospitali teule ya Wilaya Karatu na kituo cha afya cha Rhotia ambapo inaelezwa kuwa watatu walifariki dunia wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali teule na majeruhi watatu walihamishiwa Hospitali ya Mkoa wa Arusha ambapo mmoja alifariki dunia saa 10 jioni hivyo kubakia wawili ambao wote ni wasichana.
Habari kutoka kwa mashuhuda wa ajali zinadai kuwa polisi wakishirikiana na wananchi wa kijiji hicho pamoja na wapita njia walianza uokoaji mara moja baada ya kutokea kwa ajali.
Kutokana na kuharibika vibaya kwa gari hilo wananchi hao walitumia mashoka, mitarimbo, nyundo, majembe na vifaa vingine kutoa miili ya marehemu na majeruhi.
“Hali ilikuwa ya kutisha na kuogofya katika eneo la ajali, miili mingi iliyotolewa ilikuwa na majeraha makubwa ya kutisha na wengi walikuwa wamevunjika viungo vyao,” alidai mmoja kati ya waokoaji ambaye hakutaka kutajwa gazetini.
Majonzi, vilio, Mount Meru Hospitali
Hali ilikuwa ya kusikitisha katika Hospitali ya Mount Meru ambapo vilio, majonzi, simanzi vilitanda kila kona na kila mmoja wakiwamo madaktari, wauguzi, viongozi wa serikali na wa kisiasa walionekana kuguswa na tukio hilo.
Umati mkubwa wa wakazi wa Arusha na vitongoji vyake ulianza kukusanyika kuanzia saa 6 mchana baada ya taarifa kuzagaa kuwa majeruhi pamoja na miili ya waliofariki ilikuwa njia kuletwa hospitalini hapo.
Hadi kufikia saa 9 alasiri eneo lote la hospitali lilikuwa limefurika watu na barabara maarufu ya Afrika Mashariki nayo ilikuwa imefurika kiasi kwamba magari yalilazimika kupita kwa taabu.
Aidha eneo la kuhifadhia chumba cha maiti nalo lilikuwa limefurika watu ambao walikuwa wakisubiri kuona na kutambua miili ya wapendwa wao hali iliyowalazimu polisi wa kikosi cha FFU waliokuwa na silaha nzito kuimarisha ulinzi.
Ilipotimu saa 9.46 alasiri miili ya majeruhi watatu iliwasili kwa magari ya kubeba wagonjwa (ambulance) na ndipo viliposikika vilio kutoka kila kona ya viwanja vya hospitali hiyo.
Baadaye umati huo ulihamia katika eneo la chumba cha kuhifadhia maiti na miili ilipowasili polisi walishindwa kuthibiti hali kutokana na wazazi na ndugu wa marehemu kushinikiza kuwa wanataka kutambua miili ya watoto wao.
Kutokana na hali hiyo, ilimlazimu Mkuu wa Wilaya Arusha, Gabriel Dagharo, kuingilia kati na kuwataka wale tu waliofiwa waruhusiwe kuingia ndani ya chumba cha maiti kutambua miili ya watoto wao.
Kauli za viongozi
Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Dagharro, alisema binafsi na serikali amesikitishwa na msiba huo na kuongeza kuwa, serikali iko pamoja na wazazi walipoteza watoto wao.
“Msiba huu umetugusa wote, si msiba wa watu wa Arusha peke yao huu ni msiba wa taifa na ndiyo maana Rais wetu ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha na watu wote wa Arusha,” alisema.
Alisema wakati viongozi wa serikali wakikutana kufanya taratibu za mazishi kwa kusaidiana na familia ibada ya pamoja ya kuaga miili itafanyika katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid siku ya Jumatatu kuanzia saa 6 za mchana.
Kwa upande wake Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro, alisema anaungana na wazazi na wanafamilia katika kipindi hiki kigumu cha kupotea kwa maisha ya wanafunzi hao na walimu wao.
“Hakuna jambo limetuumiza watu wa Arusha kama ajali hii, natoa pole kwa wazazi na wamiliki wa shule. Naomba tuungane sote bila kujali itikadi zetu za kisiasa na imani zetu za dini huu msiba ni wetu sote watu wa Arusha na Watanzania kwa ujumla,” alisema.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Longino Vicent Nkana, aliwaambia waandishi wa habari kuwa wanafunzi hao waliondoka shuleni hapo saa 12.30 asubuhi kuelekea Karatu kwa ajili ya kushiriki mitihani hiyo ya ujirani mwema.
Alieleza kuwa wamekuwa wakifanya mitihani hiyo ya ujirani mwema kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa zaidi ya miaka mitatu sasa na hakukuwahi kutokea tatizo lolote.
“Magari yetu hufanyiwa matengenezo katika karakana zetu mbili kila wiki na yako salama na hata wakati mwingine tunakodishwa kwa shughuli nyingine za kijamii,” alifafanua.
Aliongeza kuwa shule hiyo ilianzishwa mwaka 2006 na imekuwa katika shule bora kitaaluma mkoani Arusha ambapo mwaka 2016 ilishika nafasi ya pili ngazi ya mkoa katika mitihani ya darasa la saba.
Majina ya waliofariki yaliyopatikana ni pamoja na Mteage Amos, Justine Alex, Irene Kishari, Gladness Goodluck, Praise Roland, Shadrack Biketh, Junior Mwashuye, Aisha Said, Oumligh Herri Rashid, Gema Gerald, Rebecca Daudi, Hagai Lucas, Said Ally na Ruth Ndemna.
Wengine ni Atusa Kassim, Neema Eliwashi, Neema Martine, Greyson Robson Masana, Heavennight Enock, Ian Tarimo Anold Alex, Naomia Hosea, Rukia Altam, Eliapendo Elihudi, Marion Mrema, Rehema Msuya, Sabrina Said na Prisca Charles.
Majina mengine zaidi yanatarajiwa kutolewa hapo baadaye leo.
Nitumie maoni yako Kupitia Facebook.com/proffesa nazir
Au
Nicheki == NAZIRHAMZA