Kurasa

Ijumaa, Mei 26, 2017

RAMADHANI KAREEM : Waislamu waanza kufunga kesho

Waumini wa dini ya kiislamu kote ulimwenguni wanatarajiwa kuanza kutekeleza ibada ya swaum kuanzia kesho ama kesho kutwa kulingana na kuandama kwa mwezi.
Saum ni nguzo ya nne ya dini ya kiislamu ambapo hujizuia na kula na kunywa hadi jioni pamoja na kutekeleza ibada kwa wingi.
Viongozi wa dini ya kiislamu katika kaunti ya Taita Taveta sasa wanaitaka serikali ya kitaifa kuhakikisha kuna usalama wa kutosha katika maeneo ya ibada na hasa misikiti wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhan unapoanza.
Also read:

Mahakama yahahirisha kesi ya kuwaadhibu madaktari wanaogoma

Wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza kuu la waislamu katika kaunti ya Taita Taveta Washallah Abdhi,wanasema mwezi huu ni muhimu kwa kalenda ya jamii ya waislamu na ni sharti usalama uimarishwe kuwezesha jamii hio kutekeleza ibada zao bila matatizo

Jumamosi, Mei 13, 2017

Kuhusu wenye vyeti feki kulipwa mafao


Watumishi waliobainika na vyeti feki, watalazimika kusubiri mafao yao hadi utaratibu wa kuwalipa utakapofanyika.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Amina Mollel.

Amina alitaka kujua ni hatua gani zitachukuliwa ili kuwalipa mafao yao wafanyakazi waliobainika na vyeti feki.

Waziri Kairuki alisema, ofisi yake itaandaa utaratibu wa mafao ya wafanyakazi hao na pindi utakapokamilika, watajulishwa na kulipwa haki zao.

Aidha,  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera , Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu, Anthony Mavunde, alisema kwamba seeikali inaendelea na mchakato wa kuunganisha mifuko ya jamii.

Mavunde alisema hayo alipojibu swali la msingi la Mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM), Almas Maige, aliyetaka kujua mchakato wa kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii, umefikia hatua gani.

Mavunde alisema, serikali kwa sasa inafanya tathmini ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo imetoa mapendekezo kuhusu namna bora na mambo ya kuzingatiwa katika mchakato wa kuunganisha mifuko hiyo.

Alisema, wadau vikiwemo vyama vya waajiri, vimeshirikishwa ili kutoa maoni na mapendekezo kwa serikali na kutoa maamuzi.

Proffesa J amshangaa Waziri mwakyembe kutaka wasanii wasiimbe siasa

WASIIMBE SIASA

 Saturday, May 13, 2017     burudanisiasa   

Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay, ametoa maoni yake kuhusu ushauri wa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe aliyewataka wasanii wa Tanzania kuacha kuimba nyimbo zenye jumbe za kisiasa kwani hawatafanikiwa.

Profesa Jay ambaye ni rapa nguli wa kizazi kipya aliyewahi kuweka rekodi maalum ya albam yake ya ‘Mapinduzi Halisi’ iliyokuwa na jumbe zenye mlengo wa kisiasa na kijamii, amesema ameshangazwa na kauli ya Waziri.

“Kuwaambia wasanii kuwa waimbe nyimbo za maisha yao tu na washindwe kuimba vitu vingine, maana yake unataka kutoa ‘green light’ kwa wasanii sasa waanze kuimba mambo ya mapenzi… nakupenda, nakupenda..,” alisema Profesa Jay.

“Maana yake unaweza kuchochea kuhusu masuala ya mapenzi tu na kushindwa kufanya vitu vya kijamii ambavyo vingeweza kulipeleka taifa letu mbele. Mimi naamini msanii ana sauti kubwa na anaweza kupaza sauti positively na ikasaidia taifa letu ideologically (kiitikadi), socially (kijamii), culturally (kitamaduni), economically (kiuchumi), politically (kisiasa) pamoja na sustainable development (maendeleo endelevu),”aliongeza.

Mbunge huyo alidai kuwa wapo wasanii walioimba kuhusu siasa na masuala ya kijamii kama 2Pac, BIG, Bob Marley, Lucky Dube na wengine ambao walisaidia dunia kuhama katika ngazi moja kijamii hadi ngazi nyingine.

Hata hivyo, Profesa Jay alikubaliana na hoja ya Waziri Mwakyembe kuwa wasanii hawapaswi kuitukana Serikali, akieleza kuwa wanapaswa kuachwa watoe mawazo yao mbadala ikiwa ni pamoja na kuisifia Serikali.

Akizungumza Bungeni mjini Dodoma, Waziri Mwakyembe aliwashauri wasanii kuachana na nyimbo za siasa kwani hawatafanikiwa kwakuwa hakuna msanii ambaye alijikita katika kuimba siasa na akafanikiwa. 

Kuhusu wenye vyeti feki kulipwa mafao


Watumishi waliobainika na vyeti feki, watalazimika kusubiri mafao yao hadi utaratibu wa kuwalipa utakapofanyika.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Amina Mollel.

Amina alitaka kujua ni hatua gani zitachukuliwa ili kuwalipa mafao yao wafanyakazi waliobainika na vyeti feki.

Waziri Kairuki alisema, ofisi yake itaandaa utaratibu wa mafao ya wafanyakazi hao na pindi utakapokamilika, watajulishwa na kulipwa haki zao.

Aidha,  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera , Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu, Anthony Mavunde, alisema kwamba seeikali inaendelea na mchakato wa kuunganisha mifuko ya jamii.

Mavunde alisema hayo alipojibu swali la msingi la Mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM), Almas Maige, aliyetaka kujua mchakato wa kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii, umefikia hatua gani.

Mavunde alisema, serikali kwa sasa inafanya tathmini ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo imetoa mapendekezo kuhusu namna bora na mambo ya kuzingatiwa katika mchakato wa kuunganisha mifuko hiyo.

Alisema, wadau vikiwemo vyama vya waajiri, vimeshirikishwa ili kutoa maoni na mapendekezo kwa serikali na kutoa maamuzi.

Wabunge wahuzunika sana kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha

Wakazi wa Videte Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani wakivuka mto Mzinga kwenda Bamia karibu na Uwanja wa Azam Complex Chamazi Manispaa ya Temeke Dar es Salaam. Wakazi hao wameomba kusaidiwa daraja kwa kuwa uvushaji huo ni hatari kwa maisha yao hasa kipindi hiki cha mvua. Wakazi hao wanavushwa kwa shilingi 1000 kwa kila kichwa.

0 Comments

ATHARI za mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha mafuriko na maporomoko katika sehemu mbalimbali nchini jana ziliwagusa wabunge na kutaka Bunge liahirishe shughuli zake ili wabunge waijadili hali hiyo iliyoathiri miumdobinu, makazi na hata kusababisha vifo.

Mvua hizo zinazoendelea kunyesha kwa takribani wiki tatu mfululizo sasa, zimeacha athari kubwa katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Dar es Salaam, Pwani, Tanga na Zanzibar. Wabunge walioomba mwongozo baada ya kumalizika Kipindi cha Maswali na Majibu ni Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani (CCM), Mbunge wa Vunjo James Mbatia (NCCR Mageuzi) na wa Mlalo, Rashid Shangazi (CCM).

Ngonyani maarufu kama Profesa Majimarefu alisema kuna matatizo makubwa ya mafuriko nchini. “Kwenye mkoa wangu wa Tanga kumekuwa na maafa, leo (jana) hii kuna watu 1,000 hawana chakula, mahali pa kuishi na hawana msaada wowote, lakini serikali itawasaidiaje hawa watu wakati kamati za afya zikiendelea na utaratibu,”alisema. Kwa upande wa Shangazi alitaka shughuli za Bunge ziahirishwe ili wabunge wajadili kuhusu mafuriko hayo.

“Sasa hivi katika mkoa wa Tanga kuna mafuriko makubwa sana. Jana (juzi) yametokea maporomoko katika milima ya Usambara, eneo la barabara za Lushoto- Arusha- Mombo , Pangani kwenda Tanga, Mombo kwenda Lushoto na Kilindi kwenda Morogoro zote zilifungwa,”alisema.

Alisema Mkoa wa Tanga umegeuka kuwa kisiwa umepata athari kubwa hasa Korogwe na kuiomba Serikali ilione hilo jambo ni la kimkakati na kwamba Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) amezidiwa .

Alisema barabara hizo zimekuwa zikiunganisha mkoa huo na mikoa mingine na kutaka Bunge lijadili angalau kwa muda mfupi. Naye Mbatia alisema hali ni tete kutokana na mafuriko yaliyojitokeza na kuomba utu wa mwanadamu kuzingatiwa kama wawakilishi wa Watanzania kwa kutenga muda wa angalau dakika 15 kujadili suala hilo.

“Tutenge muda wa dakika 15 ama 20 ili tujadili suala hili, ambayo ni ya maafa tunaweza tukatoa majibu sahihi kwa wapiga kura wetu, mwenyekitindio ombi langu kwa mujibu wa kanuni nilizozitumia,”alisema.

Akijibu miongozo hiyo, Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, alisema miongozo ya Mbatia na Shangazi imeangukia katika kanuni ya 47 (1) ambayo inasomwa pamoja na kanuni ya 48. “Lakini kanuni ya 47(4) inampa Spika mamlaka aridhike kama ombi hilo anaona jambo hilo kweli linahitaji kusitisha shughuli zilizo mbele yetu ili kujadili hoja hizo za dharura,”alisema.

Hata hivyo, alisema kwa hali anayoiona haoni kama suala hilo linahitaji kujadiliwa sasa. “Ni kweli tukio hili limegusa maeneo mengi, nawapa pole walioguswa kwa namna moja hata nyingine. Naamini Serikali iliyoko humu ndani itaitolea maelezo wakiangalia nchi nzima,”alisema na kuongeza kuwa, anaamini Serikali italizungumzia vizuri kuliko kila mbunge kujisemea katika eneo lake.

Kuhusu mwongozo wa Ngonyani, Chenge alisema kwa mujibu wa Kanuni ya 68 (7) ni lazima liwe tukio ama jambo ambalo limetokea mapema bungeni na si nje. Polisi asombwa, afa Wakati wabunge wakitaka kujadiliwa kwa athari za mvua zinazoendelea kunyesha, askari wa Jeshi la Polisi, Abbas Anas Haji (55) amekufa maji baada ya kusombwa akiwa na pikipiki yake aina ya Vespa wakati akipita eneo la barabara ya Fuoni Kibondemzungu lililofunikwa na maji. Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 5:30 asubuhi wakati askari huyo akitokea kazini kwenda nyumbani kwake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Nassir Ali alisema marehemu alikuwa ni mfanyakazi wa jeshi la polisi katika Kitengo cha Picha, Makao Makuu ya Polisi upande wa Zanzibar.

Familia 150 zatangatanga Katika tukio jingine, zaidi ya familia 150 kisiwani Pemba zimekosa makazi na kulazimika kusitiriwa na ndugu na jamaa baada ya nyumba zao kuathirika vibaya na mvua kubwa iliyonyesha kwa siku tatu mfululizo.

Timu ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar iliyotembelea mikoa miwili Pemba na kujionea athari za mafuriko, imeelezea kufurahishwa na mshikamano mkubwa uliooneshwa na wananchi katika kusaidiana bila ya kujali itikadi za kisiasa.

Waziri asiye na Wizara Maalumu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ali Juma Khatib alisema wananchi wameonesha uzalendo wa hali ya juu ambao watu wote walioathirika na mafuriko hayo wamehifadhiwa na kuishi kwa ndugu na jamaa.

Aidha, Khatib waliwataka wananchi walioathirika na mafuriko hayo wasirudi tena katika maeneo yao hayo ambayo athari zake bado zipo. Ameahidi kusaidia na kutoa mifuko ya saruji 50 kwa familia za wilaya ya Mkoani ili zikarabati nyumba zao.

Tanga-Arusha yafunguka Aidha, mkoani Tanga ambako miundombinu ya barabara ilisababisha kukusekana kwa usafiri kati ya mkoa wa Tanga na mikoa jirani ya Kilimanjaro na Arusha, hali imetajwa kurejea katika hali yake ya kawaida.

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Robert Gabriel akizungumza jana katika mahojiano kwa njia ya simu alisema kiasi cha mvua inayonyesha kimeanza kupungua ingawa ipo hali ya mawingu mazito katika baadhi ya maeneo.

Naye Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba akizungumzia hali ya usalama kuhusu kifusi kilichoanguka na kufunga sehemu ya eneo la barabara kuu inayounganisha miji ya Soni na Lushoto alisema anaelekea eneo la tukio na kwamba atatoa taarifa.

Aidha, kuhusu mawasiliano ya barabara ya Tanga - Pangani alisema kwa sasa watumiaji wa barabara hiyo wanapita katika njia mbili mbadala ikiwemo ya Pongwe - Kirare jijini Tanga pamoja na ile ya Muheza- Misozwe - Pangani ya wilayani Muheza wakati huu ambapo Tanroads wanafanya jitihada za kutengeneza njia ya mchepuko katika eneo la daraja la Neema lililopo kwenye barabara kuu ya Tanga- Pangani.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa ameuagiza uongozi wa Jiji la Tanga kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wajitahidi kufanya utafiti wa maeneo ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja nyakati za msimu wa mvua badala ya kiangazi ili kupata picha ya mahitaji halisi ya ujenzi tofauti na inavyofanyika sasa.

Ametoa maagizo hayo kwa nyakati tofauti jana alipozungumza katika mahojiano na HabariLeo baada ya kutembelea baadhi ya mitaa ya jijini Tanga iliyoathiriwa na mafuriko yaliyotokana na mvua isiyo ya kawaida iliyonyesha mfululizo juzi kwa saa 24 na kusababisha maafa ikiwemo vifo vya wakazi wawili.

Katika mji wa Tanga, mvua hizo ziliua watu wawili, nyumba 97 zilizingirwa maji pamoja na Soko maarufu la vyakula la Magandini na kusababisha mali zote kupotea, nyingine 36 zilibomoka kabisa, moja kutitia, nyingine kuteketea kwa ajali ya moto uliotokana na hitilafu ya umeme ambapo kaya 59 zenye wakazi zaidi ya 200 walioathirika walihifadhiwa katika kambi zilizopo kwenye shule ya msingi ya Chumbageni, Kwakaheza, Magaoni, Mafuriko na Sekondari ya Hotten.

Mvua za kihistoria Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) hivi karibuni ilitoa taarifa inayoonesha kuwa, mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali mkoani Tanga zimefikia kiwango cha juu ambacho hakikuwahi kurekodiwa tangu mwaka 1949, sawa na takribani miaka 68 iliyopita.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utafiti wa mamlaka hiyo, Dk Ladislauds Chang’a, mvua iliyonyesha kwa saa 24 Mei 9 mwaka huu mkoani Tanga ni ya milimita 316, kiwango ambacho hakijarekodiwa kwa miaka mingi.

Aliongeza kuwa, hawajafanya tathimini, lakini mwaka 2014 kulikuwa na kiwango kikubwa zaidi baada ya kunyesha mvua ya milimita 138 ndani ya saa 24 na kwamba kiwango cha juu kwa historia ya kituo cha Dar es Salaam ni mwaka 1953 iliponyesha mvua ya kiwango cha milimita 167.4. Alisema mvua za sasa zinatarajiwa kuendelea hadi mwishoni mwa mwezi huu.

Ijumaa, Mei 12, 2017

Watumishi wawili wa Serikali Mwambungu & Sozigwa waaga dunia

Mwambungu, Sozigwa wafariki dunia

IMEANDIKWA NA WAANDISHI WETUIMECHAPISHWA: 13 MAI 2017

 Kuchapa   Barua pepe

0 Comments

TAIFA limepata pigo la kuondokewa na watumishi wa Serikali wa muda mrefu, mwanahabari nguli aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Kwanza wa Rais wa Awamu ya Kwanza, Mwalimu Julius Nyerere, Paul Sozigwa na aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Saidi Mwambungu.

Wawili hao walifikwa na mauti katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) walikokuwa wamelazwa kwa matibabu. Sozigwa ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Kwanza wa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD, sasa TBC baada ya kuwa Shirika la Utangazaji Tanzania), alifikwa na mauti jana saa nane usiku wa kuamkia jana kutokana na matatizo ya moyo , wakati Mwambungu pia aliaga dunia jana asubuhi kutokana na maradhi ya figo.

Msemaji wa JKCI, Anna Nkinda alithibitisha kutokea kwa vifo vya Mzee (84) aliyekuwa amelazwa tangu Aprili 25, mwaka huu akitokea Wodi ya Mwaisela ya Hospitali ya taifa Muhimbili (MNH) na Mwambungu (62) ambaye alifikishwa hospitalini hapo Mei 10 mwaka huu saa nane mchana.

Mtoto wa kwanza wa marehemu, Hamidu Mwambungu alisema baba yake alikuwa akisumbuliwa na tatizo la figo kwa zaidi ya mwaka mmoja na ni ugonjwa ambao umemsababishia mauti hayo.

Alisema familia inaendelea kupanga taratibu za maziko. “Hatujajua mazishi yatafanyika lini na wapi bado wanafamilia tunakutana kupanga lakini nadhani tunaweza kuzika mwishoni mwa wiki hii,” alisema Hamidu. Hamidu alisema msiba huo uko nyumbani kwa marehemu Tabata Kimanga, Dar es Salaam.

Mzee Sozigwa “Mzee Sozigwa alikuwa akisumbuliwa magonjwa mengine pia, aliletwa hapa akiwa na tatizo la moyo, akatibiwa hapa akawa amepona lakini alibaki hapa wakati akiendelea na matibabu ya yale magonjwa mengine mpaka leo (jana) alipofariki,” alisema Nkinda.

Mtoto wa marehemu, Mchungaji wa Kanisa la KKKT, Moses Sozigwa alisema baba yake alikuwa akisumbuliwa na magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa moyo, matatizo ya tumbo, na pia shida mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupoteza kumbukumbu inayotokana na kuwa na umri mkubwa.

Aidha, alisema familia inaendelea kupanga mazishi ya baba yao na kwamba msiba huo uko nyumbani kwake Mtoni Mtongani, Temeke kwenye Kanisa la KKKT ambako ni maarufu kama maskani ya Kwaya ya Lulu.

Mbali ya kuwa Mkurugenzi wa RTD na baadaye mwaka 1967 kuwa Mwandishi wa Habari wa Rais, Sozigwa alikuwa kada mzuri wa chama tawala, CCM alikokuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Pwani, lakini pia akiwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho. Sozigwa atakumbukwa kutokana na weledi na uadilifu wake katika kutimiza majukumu yake.

CCM kimetoa salamu za rambirambi kwa msiba huo wa Sozigwa ambapo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole amesema kuwa chama kimepokea kwa masikitiko taarifa za msiba huo. “Mzee Sonzigwa alihudumia na kutoa huduma kwa utumishi uliotukuka ndani ya chama na pia serikali kabla na baada ya uhuru na pia alihudumia kama katibu wa kwanza wa Rais Mwalimu Nyerere,” alisema Polepole.

Alisema chama hicho kitamkumbuka na kumuenzi na jambo ambalo alishughulika nalo ni pamoja na kushughulikia misingi na maadili na miiko ya uongozi ndani ya CCM. Naye Naibu Katibu Mkuu CCM (Bara),Rodrick Mpogolo, amemtaja Mwambungu kuwa alikuwa kiongozi mwadilifu katika utendaji wake wa kazi ndani ya CCM alipokuwa Mkuu wa Utawala Makao Makuu (Ofisi Ndogo) Lumumba, Dar es Salaam na hata alipoteuliwa kuwa mtumishi wa Serikali.

“Tumempoteza kiongozi mahiri na shupavu … watu wanakumbukwa kwa yale mazuri unayofanya hapa duniani na Mwambungu atakumbukwa kwa mema aliyoyetenda wakati wa uhai wake,” alisema Mpogolo akiwa mjini hapa.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Morogoro, Christine Ishengoma, alisema alimfahamu Mwambungu wakati yeye (Dk Ishengoma) alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani mwaka 2006 na aliyekuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete.

“Nimeshistushwa na kifo chake …ninaweza kusema kuwa Mwambungu ndiye aliyenipokea wakati nikiwa mkuu wa mkoa wa Pwani na yeye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha na makao makuu ya mkoa ni Kibaha,” alisema Dk Ishengoma.

Pamoja na hayo alisema kuwa, mara baada ya Mwambungu kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa na kupangiwa mkoa wa Ruvuma, Dk Ishengoma alisema alimpokea na kukabidhi mkoa huo wakati yeye akihamishiwa mkoa wa Iringa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe, alimtaja Mwambungu kuwa licha ya kumfahamu kupitia vyombo vya habari, alifahamiana yake wakati walipoteuliwa kuwa wakuu wa mikoa.

“Mwambungu alikuwa mcheshi, alikuwa karibu na wananchi na pia ni mpenda utani ni hazina kuu imepotea, lakini ni mapenzi ya Mungu,” alisema. Baadhi ya viongozi wa CCM, wakiongozwa na Mwenyekiti wao mkoa wa Morogoro, Innocent Kalogeries na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro mjini kichama, Fikiri Juma kwa nyakati tofauti waliwajulisha wajumbe walioshiriki kikao hicho juu ya kutokea kwa msiba huo.

Momogoro blog ;watendaji wa shule ya Lucky Vincent wapandishwa kizimbani

WAKATI Mkurugenzi wa Shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Lucky Vincent ya jijini Arusha, Innocent Mushi na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Longino Nkana wakipandishwa kizimbani kutokana na vifo vya watu 35 wakiwemo wanafunzi 32 wa shule hiyo, ndege maalumu inatarajiwa kutua nchini leo kuwabeba majeruhi watatu wakatibiwe Marekani.

Mwinjilisti maarufu duniani kutoka Shirika la Samaritan Purse, Bill Graham wa Marekani na ndiye aliyebeba gharama za kukodisha ndege maalumu aina ya DC 8 kupeleka wanafunzi waliojeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita wilayani Karatu, Arusha.

Watoto hao wameumia shingo, miguu na sehemu mbalimbali za miili yao. Kwa mujibu wa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyarandu aliyezungumza jana na waandishi wa habari mjini Arusha, gharama za kukodisha ndege kwenda Marekani si chini ya dola za Kimarekani 350,000 (Sh milioni 700). Gharama hizo ni nje ya matibabu, chakula na malazi kwa wakati wote ambao wagonjwa hao na wasindikizaji watakuwa nchini humo.

“Tumefanikiwa kupata ndege aina ya DC 8 kutoka Shirika la Samaritan Purse linaloongozwa na mtoto wa Billy Graham aitwaye Franklin kwa ajili ya kuwasafirisha watoto Doreen Mshana, Sadia Awadh na Wilson Tarimo na wazazi wao watatu, yaani mama zao,” alisema Nyalandu akiwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Alisema pia watoto hao wataambatana na daktari wa hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru, Elias Mashalla na muuguzi Simphorosa Silalye. Kwa mujibu wa Nyalandu, ndege hiyo inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA) leo jioni ikitokea Charlotte ,Jimbo la North Carolina, Marekani.

“Endapo taratibu za safari ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa visa utafanikiwa, basi ndege inaondoka na wagfonjwa na wasindikizaji Jumapili (kesho) na baada ya kufika mjini Charlotte, North Carolina watasafiri kwa ndege nyingine maalumu ya kubeba wagonjwa hadi mji wa Sioux City, Iowa ambako watapokelewa na uongozi wa Hospitali ya Mercu na Shirika la STEMM,” alisema Nyalandu.

Alitumia fursa hiyo kuwataka Watanzania kupongeza juhudi za Rais, Dk John Magufuli, Makamu wake, Samia Suluhu Hassan na uongozi wa Mkoa wa Arusha chini ya Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo kwa kuguswa na kushiriki katika kila hatua kuanzia baada ya ajali, mazishi hadi ufuatiliaji wa afya za majeruhi.

‘’Hili jambo ni letu sote hapa, hatuhitaji sifa bali tunachopaswa Watanzania wote kushirikiana kwa pamoja na kuweka mbele ubinadamu na kujitoa kwa hali na mali kuwasaidia hawa watoto ili waweze kupata nafuu na kurudi shuleni,” alisema Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Gambo alisema kuwa katika michango yote iliyochangwa kwa ajili ya rambirambi kwa msiba huo mpaka jana zilipatikana fedha kiasi cha Sh milioni 215.

Gambo alisema katika fedha hizo, kila familia ilikabidhiwa zaidi ya Sh milioni 3.8 na pia Serikali ilibeba gharama za usafiri, majeneza, mafuta ya magari na malipo ya madereva. Alisema Sh milioni 190 zilitumika katika matumizi mbalimbali ya msiba huo na kuwataka walioahidi kuchangia kutimiza ahadi zao.

Kizimbani Wakati majeruhi ambao ni wanafunzi wa shule hiyo wakitarajiwa kupelekwa Marekani, mmiliki wa shule hiyo na mwalimu mkuu msaidizi walipandishwa kizimbani kwa makosa kadhaa ya usalama barabarani, ikiwa ni pamoja na kusafirisha watoto bila ya kuwa na vibali.

Wakisomewa mashitaka yao jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Hakimu Mkazi Arusha, Desdery Kamugisha, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Rose Sule alidai watuhumiwa hao wawili wamefunguliwa kesi Namba 78/2017 huku Mkurugenzi wa shule hiyo akishitakiwa kwa makosa manne na Mwalimu Nkana akishitakiwa kwa kosa moja.

Akimsomea Mkurugenzi wa Lucky Vincent makosa yake, wakili huyo alidai kosa la kwanza ni la kuendesha gari la abiria bila ya kuwa na leseni ya usafirishaji ambapo Mei 6 mwaka huu katika eneo la Kwamrombo, Arusha Mjini akiwa mmiliki wa gari namba T 871 BYS aina ya Toyota Rosa, alifanya shughuli ya usafirishaji bila ya kuwa na leseni ya abiria.

Kosa la pili ni kuruhusu kuendesha gari bila ya kuwa na bima (Road Licence), Mei 6 mwaka huu akiwa mmiliki wa gari hilo aliruhusu gari hilo kuendeshwa bila ya kuwa na bima. Kosa la tatu ni kushindwa kuingia mkataba na mwajiriwa wake, Dismas Gasper ambapo Mei 6, 2017 akiwa mmiliki wa gari alishindwa kuingia mkataba na dereva huyo aliyeendesha gari lililopata ajali ambaye naye alifariki dunia katika tukio hilo.

Kosa la nne ni kubeba abiria zaidi ya 13 ambapo Mei 6 mwaka huu, mkurugenzi huyo ambaye ni Ofisa Msafirishaji na mmiliki wa shule ya Lucky Vincent alibeba na kusafirisha abiria zaidi ya 13 katika gari hilo kitendo ambacho ni kinyume na sheria.

Kosa la tano ni la Mwalimu Mkuu Msaidizi ambapo anashitakiwa kwa kuandaa safari iliyozidi abiria 13 ambapo ni kinyume cha sheria inadaiwa kuwa Mei 6 mwaka huu, Nkana akiwa Mwalimu Mkuu Msaidizi na mwandaaji wa safari alipakia abiria zaidi ya 13 kwenye gari lililosababisha vifo vya wanafunzi hao.

Baada ya washitakiwa hao kusomewa mashitaka yao yanayowakabili wakili anayewatetea washitakiwa hao, Method Komomogolo aliomba dhamana kwa washitakiwa hao huku Wakili wa Serikali Sule akisema hana pingamizi na dhamana yao.

Hakimu Kamugisha alitoa masharti ya dhamana kwa washitakiwa hao ambayo ni kila mshitakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wawili watakaosaini bondi ya Sh milioni 15 na kwamba hawatakiwi kuondoka nchini au ndani ya mkoa bila ruhusa ya mahakama pamoja na kuwasilisha hati zao za kusafiria.

Watuhumiwa hao walitimiza masharti ya dhamana yao na kesi yao kuahirishwa hadi Juni 8, mwaka huu.

Namna ya kuamsha hisia za mwanamke

Wanaume wengi huelewa kuwa kuna umuhimu wa kumuandaa mwanamke kwa kumshika shika maungo yake ya mwili lakini wengi hupuuzia suala hili kwa kuwa wao hamasa yao ya mapenzi huamka na mwili husisimka tayari kwa kuanza kushiriki tendo la ndoa mara tu baada ya kuona mwili wa mwanamke ukiwa mtupu.

Mwanaume wa namna hii huwa hawezi kumfikisha mwanamke kwani mara baada ya kumuingilia mwanamke ambaye hayupo tayari kuingiliwa kimwili kwa kuwa hajaandaliwa, mwanaume hujikuta anafikia mshindo ndani ya sekunde kadhaa na hata akitaka kuzuia bao hushindwa kufanya hivyo, hivyo hujikuta amemaliza haja zake za kimwili na kumuacha mwanamke pengine akiwa hata wazimu haujampanda na kwa bahati mbaya aking’amua hushindwa kurudia tena tendo kwani haitasimama tena.

Wataalamu mbali mbali wa mapenzi wanabainisha ya kuwa wanaume wenye kutumia muda mwingi kumuandaa mwanamke huweza kujizuia kufika mshindo mapema na hivyo hudumu kifuani kwa muda mrefu na hata kufanikiwa mfikisha mwanamke kileleni zaidi ya mara moja.

Hata hivyo muda wa kushikana shikana hutofautiana baina ya mwanamke na mwanamke, wanawake wengi husisimka kutokana na kushikwa matiti, matiti ya mwanamke mara nyingi ni yenye kusisimka sana endapo yatatomaswa vizuri kimahaba ama kwa kutumia mikono au mdomo kupekecha chuchu mithili ya mtu anayemung’unya pipi na wazimu ukianza mpanda ncha za matiti husisimka na kujitokeza yaani hudinda na hali hiyo hujitokeza sehemu zake za siri pia kwa mashavu ya k kupanuka na kuwa na hali ya kusisimka huku kinena kikimsimama na tezi zake hutoa ute.

Ute hutoka mahususi kuruhusu uume kupenya kwa urahisi, hata hivyo si wanawake wote huamsha hamasa ya mapenzi kwa kuchezewa matiti hivyo basi mwanamke anatakiwa kumwongoza mwanaume kwa maneno ama kwa kuweka mikono eneo anataka ashikwe ili apate hamasa ya mapenzi.

Aidha, wanawake wengine huwa hawana ujasiri wa kumwongoza mwanaume kumtomasa sehemu inayomnyegesha, hivyo kujinyima raha ya mapenzi. Hivyo mwanaume anapaswa kumshika shika mwanamke sehemu mbali mbali kama shingoni, mabegani na kumbusu sehemu ya juu ya mwili wake taratibu akiteremsha mikono kwenye sehemu za siri za mwanamke lakini ahakikishe hana kucha zenye ncha na vidole vikavu ili kutomuumiza mpenziwe na kusababisha ashki impotee gafla na asitake tena mambo!

Hapa ili zoezi liwe lenye mafanikio mwanamke anatakiwa kuonyesha ushirikiano kwa kutoa miguno ya kumchanganya mwanaume huku akitanua vema miguu ili mwanaume aweze kushughulika vema na sehemu inayozunguka kinena, hadi atakapobaini mabadiliko ya moyo wa mke, ngozi kuwa na joto, pumzi kuongezeka, uso kukunjamana mithili ya mtu anayeumia na anaweza lia kwa utamu anaousikia na hapo mwanaume anaweza kumwingilia kwani huwa tayari kuingiliwa kimwili.

Askari polisi asombwa na maji unguja_zanzibar


UNGUJA: Polisi mmoja kwa jina Abbasi Anali amefariki dunia kutokana na kusombwa na maji huko Unguja, Zanzibar.

 Taarifa zilizotufikia zinaonesha kwamba askari huyo ambaye alikuwa mpiga picha wa Polisi, alikuwa akiendesha pikipiki maarufu kama Vespa, kutoka mjini Unguja kuelekea Makunduchi.

Mwandishi wa habari Bi Jazaa aliyefika katika eneo la tukio hilo anasema, “Ajali hiyo imetokea leo hii Ijumaa tarehe 12 Mei, 2017…na ilikuwa baina ya saa 5 na 6 hivi.” Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir, amethibitisha kifo cha askari huyo, na kuongeza kwamba tayari mwili wake umepatikana.

Uchunguzi wa mwili huo unaendelea katika Hospitali ya Mnazi Mmoja. “Mauti yamemfika alipojaribu kuvuka katika eneo la Kibonde mzungu, Fuoni ambapo kulikuwa na maji mengi,” Jazaa.

Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema eneo hilo lliikuwa limetapakaa maji kutokana na mvua kunyesha na kuziba barabara kuu. wanasema asakari huyo amekosa mwelekeo wakati anavuka na kutumbukia kwenye maji mengi.

Mvua kubwa inayoendelea kunyesha hasa kwenye maeneo ya ukanda wa Pwani, imesababisha madhara mengi ikiwa ni pamoja na vifo katika baadhi ya maeneo, nyumba kuanguka, magari kukwama au kuharibika, na miundombinu mingi kuharibika, hususan barabara.

Mamlaka ya Hali ya Kewa Tanzania imetoa taarifa inayoonesha ukanda wa Pwani unaendelea kupata mvua za kiasi cha 50mm ndani ya kipindi cha saa 24. Na kwakesho tarehe 13 May, 2017, “kuna Angalizo la Matarajio ya kuwepo Vipindi vifupi vya Mvua kubwa,” Kwa mujibu wa taarifa za tovuti yao.

Kwa upande wa Zanzibar, maeneo yaliyoharibika zaidi ni pamoja na Mwanakwerekwe, Kibonde mzungu, Ziwa maboga, Mtoni kidato, Jeng’ombe, na Sebleni kwa wazee.

Nitumie maoni yako kwa kubonyeza Jina ilo apo chini
NazirHamza

Jambazi wakike auawa jijini Nairobi

Katika Facebook, mwanamke huyo anajitambulisha kama mwanafunzi wa zamani wa chuo kikuu


Mwanamke anayedaiwa kuwa jambazi sugu, ambaye amekuwa akipakia mtandaoni picha zake akiwa amejipodoa na kujipamba, ameuawa na polisi jijini Nairobi nchini Kenya.

Kijana huyo ambaye ametambuliwa kama Claire Mwaniki aliuawa na polisi alfajiri na mapema Jumatano katika mtaa wa kayole.

Gazeti la kibinafsi la Daily Nation linasema mwanamke huyo alikuwa na majambazi wengine wanne wa kiume pale walipofumaniwa na polisi wakitekeleza wizi katika eneo la Lower Chokaa, mtaa wa Kayole.

Anadaiwa kufyatulia risasi maafisa wa polisi akiwa na jambazi mwingine lakini wawili hao wakauawa.

Wenzao walifanikiwa kutoroka.

Taarifa katika gazeti la Daily Nation inasema polisi waliwaandama baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wenzao kupitia WhatsApp kwamba majambazi hao walikuwa wamekwepa mtego waliokuwa wamewekewa.

Polisi walijiandaa na kisha wakawakabili katika mtaa wa Lower Chokaa.

Mkuu wa polisi wa mtaa wa Kayole Joseph Gichangi amenukuliwa na gazeti la Daily Nation akisema: "Kwa mujibu wa wadokezi wetu, mwanamke huyo alikuwa mke wa mshukiwa wa ujambazi ambaye anafahamika vyema, ambaye bado anasakwa na polisi."

Alisema visa vya wanawake kujihusisha na magenge yanayotekeleza wizi wa kutumia mabavu vinaongezeka.

Wakenya mtandaoni wamekuwa wakisambaza picha za Mwaniki na kumjadili sana mtandaoni.

Katika Facebook, mwanamke huyo anajitambulisha kama mwanafunzi wa zamani wa chuo kikuu cha Nairobi na mtu anayependa kufurahia maisha.

Kuna wakati alipakia picha yake, ya mwanamume na mtoto, na kuongeza kwamba hiyo ni "familia".

Mkuu wa polisi Nairobi Japheth Koome anasema magenge mengi ya wahalifu huwa na wanawake.

"Wanawake hutumiwa kusafirisha silaha, kukusanya habari na hata kushiriki katika ujambazi," Bw Koome alisema.

Aliongeza kuwa wakati mwingine hutumiwa na majambazi wa kiume kuwapelekea chakula mafichoni.

Nitumie maoni yako Kupitia
Facebook kwa kubonyeza Jina ilo apo chini  Nazir-Hamza

Betri za simu aina ya smartphone zinazochaji simu ndani ya dk 5

StoreDot walitoa mfano wa siku ikiwekwa chaji kwa kutumia chaja maalum

Betri za simu za kisasa za Smartphone ambazo zinaweza kujaa chaji katika muda wa dakika tano pekee huenda zikaanza kuuzwa sokoni mwaka ujao.

Teknolojia hiyo iliwekwa kwenye maonesho mara ya kwanza mwaka 2015 na kampuni ya Israel ya StoreDot.

Kampuni hiyo iliwasilisha kwenye maonesho ya kila mwaka ya teknolojia mpya ya CES mjini Las Vegas betri hiyo maalum iliyopewa jina FlashBattery.

Afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Doron Myersdorf ameambia BBC kwamba sasa wanatarajia kuanza kuzalisha na kuuza betri hizo mapema mwaka 2018.

Hata hivyo, Ben Wood, mchanganuzi wa teknolojia katika kampuni ya CCS Insight amesema ana shaka kidogo kuhusu ahadi hiyo.

Bw Myersdorf amesema hawezi kufichua kwa sasa ni kampuni gani ambazo zimepata idhini ya kutengeneza betri kwa kutumia teknolojia hiyo.

Mwaka 2015, aliambia BBC kwamba betri hizo za kampuni yake zimeundwa kwa kutumia viungo ambavyo vinawezesha kufanyika kwa shughuli za kemia kwa haraka isiyo ya kawaida na pia kuhamishwa kwa nguvu za umeme kutoka sehemu moja hadi nyinginwe kwa kasi sana.

Baadhi ya miundo ya betri hizo ilikuwa kubwa kuliko betri nyingi za smartphone za wakati huo, lakini Bw Myersdorf anadai sasa wameandaa betri ambazo zinaweza kuanza kuuzwa sokoni.

"Tutachaji simu ya smartphone kwa dakika tano," alisema.

Aliongeza kwamba teknolojia hiyo tayari inafanyiwa majaribio na watengenezaji betri wawili China na kwamba utengenezaji kwa wingi wa betri hizo unatarajiwa kuanza robo ya kwanza ya 2018.

Lakini ingawa Bw Wood ana shaka kwamba betri hizo zinaweza kuuzwa haraka hivyo, amekiri kwamba iwapo betri hizo zitafanya kazi kama ilivyoahidiwa, basi utakuwa ni ufanisi mkubwa sana katika sekta hiyo.

"Kubahatisha kuhusu teknolojia ya betri kunaweza kukudhuru. Nimejifunza kuwa na shaka kila wakati kuhusu ahadi hizi. Hebu tusubiri," aliambia BBC.

Alieleza kuwa muundo wowote ambao unatoa joto kwa wingi unaweza kuathiri utendakazi wa betri.Dot pia wanadai wameunda betri ya gari inayoweza kujaa chaji kwa dakika tano pekee

Kuna kampuni nyingine zinazojizatiti kuunda betri ambazo zinajaa chaji kwa haraka.

Novemba, Qualcomm walitangaza betri za Quick Charge 4 ambazo zinaahidi betri hiyo itajaa chaji kwa dakika tano na kusalia na chaji kwa saa tano.

StoreDot pia walizindua betri ya gari ambayo inajaa chaji kwa dakika tano katika maonesho ya teknolojia mjini 

TANESCO YATOA OMBI KWA WANANCHI WOTE


SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limewaomba wateja wake na wananchi kwa ujumla kutoa taarifa mapema mara inapotokea hitilafu ya umeme iliyosababishwa na mvua au sababu nyingine.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2017, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (pichani juu), alisema, sambamba na hilo pia wananchi wasifanye shughuli au kukaa chini ya miundombinu ya umeme.

“Lakini tunawaomba wananchi watoe taarifa haraka maeneo yenye mafuriko au mkusasnyiko wa maji mengi ili wataalamu wetu waweze kuchukua hatua za haraka.” Alisema.

Dkt. Mwinuka pia alisema endapo kuna nyaya, nguzo au kifaa chochote cha umeme kimepata hitilafu na kinahatarisha maisha ni vema uangalizi au alama ikawekwa ili kuwapa hadhari wapiti njia na watoto wasikaribie eneo hilo wakati mafundi wa TANESCO wakichukua hatua za marekebisho.

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA), katika taarifa yake iliyotoa Mei 9, 2017 imeonya kuwa maeneo ya Pwani ya Kaskazini ikiwemo visiwa vya Unguja na Pemba, yatakabiliwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24 kuanzia Mei 10 hadi 12, 2017.

 Aidha kwa upande wake, mtaalamu wa masualaya umeme kutoka TANESCO, Mhandisi Simon Kihiyo, amewahakikishia wananchi kuwa miundombinu ya TANESCO iko imara na salama, na hitilafu zinazotokea za hapa na pale nyingizinasababishwa na sababu za kibinadamu, au za kimazingira kama vile nguzo za umeme kugongwa na magari, au miti kuangukia nguzo. 

"Naomba nitoe angalizo kwa wateja wetu, kama pametokea hitilafu yoyote ya umeem nyumbani kwako, ni vema ukatoa taarifa TANESCO au ukamtafuta fundi wa umeme mwenye taaluma badala ya kushughulikia tatizo hilo wewe mwenyewe ilihali ukiwa huna utaalamu na masuala ya umeme, kwani hiyo ni hatari."

Naye kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO Leila Muhaji amesema, katika kipindi hiki cha mvua kuna athari ndogo ndogo zimetokea kwenye miundombinu ya TANESCO hususan nguzo za umeme, lakini akatoa hakikisho kuwa mafundi wa TANESCO wanekuwa wakichukua hatua za haraka kurekebisha athari katika miundombinu ya umeme pindi tu zinapotokea.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (katikati), akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Me11, 2017. Dkt. Mwinuka ametoa hadhari kwa wananchi kutogusan miundombinu ya Tanesco hususan nyaya zilizoanguka, au kufanya shughuli yoyote karibu na miundombinu yab umeme katika kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendela kunyesha nchini. Kulia ni Mhandisi Simon Kihiyo, na kushoto ni Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji.



Mhandisi Simon Kihiyo, akitoa ufafanuzi wa kitaalamu kuhusu hatua za kuchukua pindi hitilafu ya umeme inapotokea

Dkt. Mwinuka (kushoto) na Mhandisi Kihiyo, wakati wa mkutano huo leo

Dkt. Mwinuka akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake

Waandishi wa habari wakiwa kazini

Waandishi wa habari wakiwa kazini

Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, akitoaufafanuzi zaidi wa hatua za kuchukua endapo wateja au wananchi wataona hitlafu ya umeme kwenye maeneo yanayowazunguka

Mhandisi Kihiyo, (kulia0na Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO Leila Muhaji katika mkutano na wanahabari

Mhandisi Simon Kihiyo, (kulia), Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji (kushoto) na Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Henry Kilasila wakijadiliana jambo.

Alhamisi, Mei 11, 2017

Polisi yadaka mwanafunzi akifanya njama ya kuuza bastora

Bastola

0 Comments

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia mwanafunzi wa Chuo cha St Joseph, Lewis Mbise (23) akituhumiwa kukutwa na bastola moja aina ya Luger cz 100 yenye namba C 4122 ikiwa na risasi 13 ndani ya magazine, mali ya baba yake kwa lengo la kuiuza.

Pia linawashikilia walimu wawili na mwanafunzi kwa tuhuma za kuvujisha mtihani wa Kidato cha Sita unaoendelea. Akizungumzia tukio la mwanafunzi kukamatwa na bastola, Kamanda wa kanda hiyo, Kamishna Simon Sirro aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba mwanafunzi huyo alisema alikamatwa Mei 5 maeneo ya Mbezi Magari Saba katika Manispaa ya Ubungo baada ya kupata taarifa kuwa kuna kijana anauza silaha.

Kamanda Sirro alisema baada ya taarifa hizo, jeshi hilo lilifuatilia na kumpata kijana huyo na katika mahojiano, alikiri kuwa bastola hiyo aliiba nyumbani kwa baba yake mzazi pamoja na fedha kiasi cha Sh 800,000. “Ni watu wengi wanatumia silaha, lakini hawatunzi silaha ni kitu ambacho kinatakiwa kutunzwa.

Tayari nimeagiza baba wa kijana huyu akamatwe kwa hatua zaidi, niwasihi na wengine wanaotumia silaha kuhakikisha silaha hizo zinahifadhiwa vizuri,” alieleza Kamanda Sirro. Alisema upelelezi unaendelea kufanyika ili kubaini lengo la mtuhumiwa kuiba silaha hiyo ikiwamo kujua kama kuna taarifa ya kupotea kwa silaha hiyo kabla haijapatikana.

Sirro alisema watuhumiwa waliokamatwa kwa tuhuma za kuvujisha mitihani ni walimu Musa Elius (35) na Innocent Mrutu (33) mkazi wa Kibamba na mwanafunzi Ritha Mosha.

Kamanda Sirro alisema watuhumiwa hao walinaswa Mei 6, maeneo ya Chang’ombe baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Ofisa wa Baraza la Mitihani la Taifa, Aron Mweteni kuwa Mei 5, katika Shule ya Sekondari Chang’ombe alimkuta Elius akiingia darasani na mwanafunzi Mosha ambaye ni mtahiniwa wa mtihani wa Kidato cha Sita unaoendelea, wakiwa na karatasi yenye maswali na majibu ya somo la Kemia kwa Vitendo.

Alisema baada ya kuwakamata na kuwatilia shaka, ufuatiliaji wa awali ulifanyika kupitia Baraza la Mitihani la Taifa na kubainika kuwa swali hilo ni miongoni mwa maswali ya mitihani ya Kidato cha Sita unaofanyika mwaka huu.

Mitihani hiyo ilianza Mei 2, mwaka huu na itakamilika Mei 19, mwaka huu. Kamanda Sirro alisema watuhumiwa wote wanaendelea na mahojiano na upelelezi utakapokamilika watachukulia hatua za kisheria.

Marubani kutoka Tanzania wapata ujuzi namna ya kuendesha ndege

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt. Agustine Mahiga akizungumza wakati wa mkutano baina ya wawakilishi kutoka Tanzania na Afrika Kusini kuhusu majadiliano ya awali ya mikataba na makubaliano ya ushirikiano baina ya Tanzania na Afrika Kusini yanayotarajiwa kutiwa saini kesho wakati wa Ziara ya Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini anayetarajiwa kuwasili leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Afrika Kusini Maite Nkoana – Mashabane

SERIKALI ya Jamhuri ya Afrika Kusini imekubali kuendelea kuwafudisha marubani wa Tanzania ikiwa ni sehemu moja wapo ya kukuza maendeleo ya sekta ya uchukuzi na usafiri wa anga pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Augustine Mahiga ameyabainisha hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa  ufafanuzi kuhusu majadiliano ya awali yaliyofanyika kati ya nchi hizo mbili juu ya mikataba mbalimbali inayotegemewa kusainiwa Mei 11 mwaka huu.

Balozi Mahiga alisema kuwa katika majadiliano hayo wamejadili mikataba iliyowahi kusainiwa kwa kupima utekelezaji wake pamoja na kujadili mikataba mipya iliyojikita katika sekta mbalimbali za maendeleo zikiwemo za uchukuzi, nishati, elimu pamoja na mawasiliano.

“Katika sekta ya uchukuzi tumekubaliana kuboresha barabara, usafiri wa anga pamoja na reli hasa ya TAZARA, sisi tumenunua ndege na tunaendelea kununua zingine zitakazosafiri hadi Afrika ya Kusini hivyo nchi hiyo imekubali kuendelea kuwafundisha marubani wa Tanzania kuendesha na kukarabati ndege hizo,”alisema Balozi Mahiga.

Nitumie maoni yako Kupitia
Fb.com

Jumatano, Mei 10, 2017

Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule ya Lucky Vincent huko karatu atafakari saa Mara mbili

1 Comment

MWALIMU Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi ya mchepuo wa Kiingereza ya Lucky Vincent ya jijini Arusha, Loningo Vincent amesema kabla ya kuanza safari ya kwenda Karatu ambayo iliibua ajali iliyoua wanafunzi 33, walimu wawili na dereva, alitafakari kwa saa mbili waende huko au Njiro jijini humo kwa ajili ya mtihani wa kujipima.

Wanafunzi hao 33, walimu wao wawili na dereva walikufa baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Mitsubishi Rosa kupinduka na kutumbukia korongoni eneo la Mlima Rhotia Marera wilayani Karatu wakati wakienda katika mtihani wa ujirani mwema wa kujipima na wenzao wa Tumaini Junior.

Akizungumza wakati wa maziko ya mwanafunzi Irene Godson jana, Mwalimu Vincent aliomba samahani kwa wazazi na walezi kutokana na ajali iliyotokea ambayo si tu imeacha simanzi kubwa kwa familia husika, bali Taifa kwa ujumla.

Alisema kabla ya kuondoka shuleni hapo, alitafakari sana ndani ya saa mbili watoto hao waende Njiro jijini Arusha au Karatu kufanya mtihani wao wa kujipima. “Kabla ya watoto hawa kuondoka, nilitafakari saa mbili kama waende Karatu au Njiro hapa hapa mjini, lakini sikuwa najua kama wanakwenda kufa, wazazi mtusamehe maana hakuna aliyejua mbele kuna nini kitatokea,” alisema Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Lucky Vincent.

“Naomba nikabidhi kitabu hiki cha nyimbo za dini ambacho Irene alikuwa nacho kwenye begi Lake na walipopata ajali Irene alijitaja mara tatu kwa jina lake Irene, Irene, Irene. Kweli alikuwa akipenda sana dini kwa sababu pia ndani ya begi lake alikuwa na mafuta ya mzeituni yaliyowamwagikia wenzake wakati kila mmoja akiwa kwenye harakati za kujiokoa,” aliongeza mwalimu huyo.

Awali kabla ya kuanza ibada, Mwalimu Vincent alikabidhi Biblia kwa wazazi kwani Irene alikuwa ni mcha Mungu na kila mara alikuwa na Biblia yake na hata eneo la ajali, walimu waliokota biblia hiyo.

“Irene alikuwa ni mcha Mungu na sehemu aliyopata ajali alikuwa na Biblia yake na alikuwa akimtumaini mungu kwa kila jambo, hivyo kama walimu tunaikabidhi Biblia hii kwa familia yake,” alieleza mwalimu huyo.

Mamia ya watu walijitokeza nyumbani kwa wafiwa Kwamrombo Murriet kwa ajili ya kumuaga Irene ambaye mwili wake ulipowasili nyumbani kwa bibi na babu yake saa 6.15 mchana vilio, huzuni na simanzi vilitawala, huku bibi yake akilia zaidi kutokana na jinsi alivyokaa naye tangu akiwa na miaka miwili hadi juzi mauti ilipomfika.

Akiongoza Ibada ya mazishi, Mchungaji kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Asisisa Moshi kutoka Ushirika wa Olkerian alitoa pole kwa familia. Naye Askofu Solomon Masangwa wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini alitoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki waliokumbwa na msiba huo na kuwasihi wazazi kumwachia Mungu kwani hayo ni mapenzi yake Irene alizaliwa Mei 5, 2004, alisoma Shule ya Lucky Vincent na alipata ajali Mei 6, 2017 eneo la Rothia.

Juzi miili ya watoto hao iliagwa kwa pamoja huku mengine ikisafirishwa na mengine ikienda kuzikwa maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha, ambapo Hospitali ya Selian miili iliyobaki ikisubiri taratibu za mazishi ikiwa ni miwili ambayo ni mwili wa Iyan Tarimo na Irene Kishari.

Mjini Dodoma, Mwandishi Wetu, Maulid Ahmed anaripoti kuwa Serikali imeliagiza Jeshi la Polisi nchi nzima kuanzia sasa kukagua magari yote yanayosomeka kuwa ni ya wanafunzi. Sambamba na hilo, Polisi wamegizwa kukagua madereva wote wanaoendesha magari ya wanafunzi kuhakikisha magari hayo ni salama ili kuwalinda watoto.

Akijibu hoja za wabunge, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni alisema serikali imechukua uamuzi huo kutokana na ajali iliyotokea Arusha na kuua wanafunzi wasio na hatia

Rais Jackob Zuma atua nchini ikiwa ni ziara yake ya 3

Dar es Salaam. Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amewasili nchini leo (Jumatano) usiku.

Rais Zuma atakuwa nchini kwa ziara ya siku tatu kufuatia mwaliko kutoka kwa Rais John Magufuli.

Ziara ya Rais huyo hapa nchini inalenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini.

Katika ziara hiyo Rais Zuma anatarajiwa kushiriki mkutano wa wafanyabiashara, kuzindua jengo la Ubalozi wa Afrika Kusini na kutembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Mkuu wa Mkoa ubungo aonya vikali juu ya kujisaidia kwenye chupa

MKUU wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori, amesema viongozi wa masoko, mitaa na maeneo ya kazi hasa masoko wanapaswa kusimamia sheria ili kudhibiti wanaochafua mazingira kwa kujisaidia katika chupa za maji na kuzirusha katika makazi au maeneo wazi.

DC Kisare alisema hayo hivi karibuni baada ya kupokea malalamiko ya wananchi waliosema baadhi ya wafanyabiashara katika Soko la Simu 2000 lililopo Ubungo Dar es Salaam, wanajisaidia haja ndogo katika chupa kisha kuzirusha katika mitalo na maeneo mengine ya wazi yakiwamo makazi ya watu na barabarani.

Mkuu wa Wilaya alisema bila wafanyabiashara hao kutambua umuhimu wa usafi, kutunza mazingira na uongozi wa soko kuchukua hatua makini, ipo hatari ya kuibuka magonjwa ya mlipuko ukiwamo ugonjwa wa kipindupindu.

“Viongozi wa masoko na maeneo wana wajibu wa kusimamia usafi na kuchukua hatua za kisheria kwa wanaokwenda kinyume maana kusambaza uchafu kama huo ni kosa la jinai kwa sababu mtu anayefanya hivyo anasababisha usumbufu, kero na kuhatarisha afya na maisha ya watu,” alisema DC Kisare.

Rukia Wandwi, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni alisema, “Hali hiyo inasababisha kero na inaweza kuhatarisha afya na maisha ya watu maana baadhi ya wamachinga pale, wanajisaidia katika chupa za maji kisha wanazirusha katika uzio. Sasa unakuta asubuhi watu tunafanya kazi ya kuokota chupa hizo zilizowekwa choo ndogo.”

Watu 5 wapoteza maisha kwa kuangukiwa na mti kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha

FAMILIA ya Jonathan Kalambwia (55) wa Kata ya Sokoni II, Kijiji cha Ng’iresi wilayani Arumeru imepoteza watoto wake wote watano wakiwemo wanafunzi wawili kutokana na athari za mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo ya mkoa huo.

Tukio hili limetokea wakati simanzi na majonzi ya vifo vya wanafunzi 33 na watumishi watatu wa Shule ya Lucky Vincent ya Arusha zikiendelea, majonzi yameukumba tena Mkoa wa Arusha baada ya Saa saba usiku wa kuamkia jana, katika eneo hilo la Ng’iresi mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mfululizo mkoani hapa, zilisababisha maafa kwa familia ya Kalambwia baada ya mti uliokuwa katika mlima Lake Mana kung’oka na kuangukia nyumba ya mzee huyo iliyokuwa chini ya mlima huo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Charles Mkumbo (pichani) alisema kati ya watoto hao watano, wawili ni wanafunzi. Baba yao ni mlinzi wa Hospitali ya Dk Mohamed ya jijini Arusha. Kamanda Mkumbo aliwatajaja wanafunzi ambao ni watoto wa Kalambwia ambaye siku ya tukio alikuwa kazini ni Miriam Jonathan (16) wa Kidato cha Pili wa Shule ya Sekondari ya Inaboishu na Gloria Jonathani (11) ambaye ni wa Shule ya Msingi Ng’iresi iliyoko wilayani Arumeru.

Alisema watoto wengine waliokufa ni mtoto wa kwanza, Giliad Jonathan (31), Lazaro Jonathan (26) na Best Jonathan (20). Mama wa watoto hao hakuwapo wakati wa ajali hiyo. Kamanda Mkumbo alisema mti huo uliokuwa katika mlima wa Lake Mana uliangukia nyumba hiyo baada ya kung’olewa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika Jiji la Arusha na mkoa kwa ujumla.

Aliipa pole familia ya mzee huyo kwani tukio hilo ni majonzi makubwa kwake kwani familia nzima imeondoka na kumtaka kuwa na uvumilivu. Kamanda Mkumbo alitoa mwito na ushauri kwa wakazi wa Arusha kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa kukarabati nyumba zao na kuacha kujenga chini ya mti ama kwenye vyanzo vya maji.

Alisema kujenga katika vyanzo vya maji ama chini ya mti ni kujitafutia majanga mengine hivyo ni vema kila mkazi wa Mkoa wa Arusha kuchukua tahadhali hiyo.

Mkuu wa Mkoa ubungo aonya vikali juu ya kujisaidia kwenye chupa

MKUU wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori, amesema viongozi wa masoko, mitaa na maeneo ya kazi hasa masoko wanapaswa kusimamia sheria ili kudhibiti wanaochafua mazingira kwa kujisaidia katika chupa za maji na kuzirusha katika makazi au maeneo wazi.

DC Kisare alisema hayo hivi karibuni baada ya kupokea malalamiko ya wananchi waliosema baadhi ya wafanyabiashara katika Soko la Simu 2000 lililopo Ubungo Dar es Salaam, wanajisaidia haja ndogo katika chupa kisha kuzirusha katika mitalo na maeneo mengine ya wazi yakiwamo makazi ya watu na barabarani.

Mkuu wa Wilaya alisema bila wafanyabiashara hao kutambua umuhimu wa usafi, kutunza mazingira na uongozi wa soko kuchukua hatua makini, ipo hatari ya kuibuka magonjwa ya mlipuko ukiwamo ugonjwa wa kipindupindu.

“Viongozi wa masoko na maeneo wana wajibu wa kusimamia usafi na kuchukua hatua za kisheria kwa wanaokwenda kinyume maana kusambaza uchafu kama huo ni kosa la jinai kwa sababu mtu anayefanya hivyo anasababisha usumbufu, kero na kuhatarisha afya na maisha ya watu,” alisema DC Kisare.

Rukia Wandwi, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni alisema, “Hali hiyo inasababisha kero na inaweza kuhatarisha afya na maisha ya watu maana baadhi ya wamachinga pale, wanajisaidia katika chupa za maji kisha wanazirusha katika uzio. Sasa unakuta asubuhi watu tunafanya kazi ya kuokota chupa hizo zilizowekwa choo ndogo.”

Watu 5 wapoteza maisha kwa kuangukiwa na mti kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha

FAMILIA ya Jonathan Kalambwia (55) wa Kata ya Sokoni II, Kijiji cha Ng’iresi wilayani Arumeru imepoteza watoto wake wote watano wakiwemo wanafunzi wawili kutokana na athari za mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo ya mkoa huo.

Tukio hili limetokea wakati simanzi na majonzi ya vifo vya wanafunzi 33 na watumishi watatu wa Shule ya Lucky Vincent ya Arusha zikiendelea, majonzi yameukumba tena Mkoa wa Arusha baada ya Saa saba usiku wa kuamkia jana, katika eneo hilo la Ng’iresi mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mfululizo mkoani hapa, zilisababisha maafa kwa familia ya Kalambwia baada ya mti uliokuwa katika mlima Lake Mana kung’oka na kuangukia nyumba ya mzee huyo iliyokuwa chini ya mlima huo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Charles Mkumbo (pichani) alisema kati ya watoto hao watano, wawili ni wanafunzi. Baba yao ni mlinzi wa Hospitali ya Dk Mohamed ya jijini Arusha. Kamanda Mkumbo aliwatajaja wanafunzi ambao ni watoto wa Kalambwia ambaye siku ya tukio alikuwa kazini ni Miriam Jonathan (16) wa Kidato cha Pili wa Shule ya Sekondari ya Inaboishu na Gloria Jonathani (11) ambaye ni wa Shule ya Msingi Ng’iresi iliyoko wilayani Arumeru.

Alisema watoto wengine waliokufa ni mtoto wa kwanza, Giliad Jonathan (31), Lazaro Jonathan (26) na Best Jonathan (20). Mama wa watoto hao hakuwapo wakati wa ajali hiyo. Kamanda Mkumbo alisema mti huo uliokuwa katika mlima wa Lake Mana uliangukia nyumba hiyo baada ya kung’olewa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika Jiji la Arusha na mkoa kwa ujumla.

Aliipa pole familia ya mzee huyo kwani tukio hilo ni majonzi makubwa kwake kwani familia nzima imeondoka na kumtaka kuwa na uvumilivu. Kamanda Mkumbo alitoa mwito na ushauri kwa wakazi wa Arusha kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa kukarabati nyumba zao na kuacha kujenga chini ya mti ama kwenye vyanzo vya maji.

Alisema kujenga katika vyanzo vya maji ama chini ya mti ni kujitafutia majanga mengine hivyo ni vema kila mkazi wa Mkoa wa Arusha kuchukua tahadhali hiyo.

Jumanne, Mei 09, 2017

Ajali Arusha

Huyo ni miongoni mwa wale wanakwenda kupumzika katika nyumba ya milele

R. I. P KWA WALIOPOTEZA wapendwa inasikitisha sana
R. I. P
Ajali Arusha

RAIS JOHN POMBE MAGUFULI ASIKITIKA SANA KUTOKANA NA AJALI ILIYOTOKEA KARATU_MKOANI ARUSHA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ametoa neno na kusema amepatwa na uchungu na majonzi baada ya kuona majeneza ya watoto na walezi wao ambao walipata ajali ya basi huko Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.


Rais Magufuli amesema hayo kupitia ukurasa wake wa twitter na kuwataka Watanzania kuomboleza msiba huu kwa umoja huku tukiwaombea marehemu hao wapumzike mahali pema peponi.

"Nimepatwa na uchungu na majonzi makubwa ninapoyaona majeneza ya watoto na walezi wao waliopoteza maisha katika ajali ya basi huko Arusha, tumewapoteza mashujaa wetu katika elimu. Tuwaombee na tuendelee kuwa na subira, uvumilivu na ustahimilivu, tunapoomboleza vifo vya wapendwa wetu tuendelee kuwa wamoja. Mungu ibariki Tanzania" alisema Rais Magufuli 

Mbali na hilo miili yote ya marehemu ambayo imeagwa leo katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha imesafirishwa na kuelekea sehemu mbalimbali za nchi kwa ajili ya ndugu kufanya maziko ya wapendwa wao hao.  

UKUMBI WA MAHABA

HAKUNA kitu kizuri kama ukiwa kwenye uhusiano, unaoonyesha dalili zote za mafanikio kwa maana ya maelewano, masikilizano, kuheshimiana lakini kubwa zaidi uliotawaliwa na amani na upendo.

Jambo la msingi watu wanapaswa kulifahamu ni kwamba, wengi wetu huharibu wenyewe uhusiano tulionao kutokana na matendo yetu. Lakini pamoja na hayo, zipo njia zinazoweza kusaidia kulinda uhusiano, usiingie dosari na kuvurugika, kukosa maelewano lakini baya zaidi kuvunjika.

Jambo la kwanza la msingi ili kuulinda uhusiano wako si kwa mwanamume au mwanamke, ni upendo. Kila aliye katika uhusiano ahakikishe anamuonyesha mwenza wake upendo wa dhati na si kusubiri yeye ndio aonyeshwe upendo.

Kumbuka kumuonyesha mtu upendo si lazima umwambie unampenda kila saa au kila dakika la hasha, unaweza kumuonyesha mwenza wako upendo kwa vitendo tu. Mfanyie mambo ambayo unajua fika yatamfurahisha na yatamuonyesha dhahiri namna unavyomjali na kumpenda.

Pamoja na hayo, jambo lingine linalochangia kulinda uhusiano wako, ni kuhakikisha una msiri na mambo yenu ya ndani. Wengi hapa huvuruga kwa kutoa kila kitu cha uhusiano wao hadharani. Hali hii kwa kweli ni mbaya na inaweza kuvunja uhusiano husika.

Si jambo la ajabu kukuta wenza wanatukanana hadharani na kudhalilishana au kusimulia kwa mashoga na marafiki kila kinachojiri ndani ya uhusiano huo. Kumbuka si kila mtu anafurahia uhusiano ulionao, hivyo

Nitumie maoni yako kwa kubonyeza hapo chini

Nazir-Hamza

TAIFA LALIA

JIJI la Arusha na vitongoji vyake jana lilisimama kwa simanzi, majonzi na vilio kwa zaidi ya saa tano wakati wa ibada maalumu ya maziko ya kitaifa ya wanafunzi 33 wa darasa la saba, walimu wawili na dereva mmoja wa Shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Lucky Vincent ya jijini Arusha waliokufa kwa ajali ya gari Jumamosi asubuhi.

Hali ilikuwa mbaya pale miili 35 iliyokuwa ikitolewa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kupelekwa kwenye Uwanja wa Michezo wa Shehe Amri Abeid Kaluta ambako ibada hiyo ilifanyika ikiongozwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan. Maiti hizo zilikuwa katika magari maalumu matatu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yenye namba za usajili 5611JWTZ08 aina ya IVIECO, gari lingine la jeshi hilo aina ya Ashok Leyland lenye namba za usajili 9123JWTZ na gari la tatu ni la aina hiyo hiyo lenye namba za usajili 9121JWTZ.

Msafara wa magari hayo ulianza saa 2.10 asubuhi kutoka Hospitali ya Mount Meru, lakini uliingia Uwanja wa Sheikh Amri Abeid saa 5.15 asubuhi, saa tatu zaidi kutokana na umati wa watu kuangua vilio barabarani pindi maiti hizo zilipokuwa zikipita na wengine kuzuia magari hayo kupita bila ya kujitambua kuwa wanafanya makosa. Askari wa JWTZ kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Arusha ilibidi wafanye kazi ya ziada kuwaondoa watu hao barabarani waliokuwa wakigalagala kwa vilio na kuwasogeza ili maiti hizo zipite na kuelekea uwanjani ambako uwanja huo unaochukua watu zaidi ya 15,000, lakini ulijaa pengine maradufu ya uwezo wake.

Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ilibidi kufanya kazi ya ziada kuwaasa wananchi wa Arusha kuruhusu magari hayo ya jeshi kupitia na kusiweze kutokea majanga mengine yasiyokuwa na msingi. Hali ya vilio na majonzi ilizidi zaidi pale miili hiyo ilipoingia kwenye uwanja huo wa michezo saa 11.15 asubuhi na kufanya watu zaidi ya 155 wakubwa kwa wadogo wakiwemo wanafunzi, kuanguka kwa kuzirai baada ya kupatwa na mshituko walipoona maiti zikiwa katika majeneza zikiingia uwanjani hapo.

Kwa mujibu wa Chama cha Msalaba Mwekundu Mkoa wa Arusha, watu zaidi ya 200 walizirai katika ibada hiyo ya jana. Magari ya kubeba wagonjwa yalilazimika kufanya kazi ya ziada kubeba wagonjwa waliokuwa wakianguka uwanjani na kuwakimbiza Mount Meru kupata matibabu ya awali. Maiti hizo zilipofikishwa uwanjani, ziliteremshwa kwa ustadi mkubwa na askari wa JWTZ kwa kushirikiana na vijana wa Skauti na kupelekwa uwanjani sehemu ilipotengwa kwa ajili ya ibada ya kuaga wanafunzi, walimu na dereva huyo waliokufa katika ajali ya barabarani eneo la Rhotia Marera wilayani Karatu wakati basi lao aina ya Mitsubishi Rosa lilipotumbukia korongoni wakiwa safarini kwenda wilayani humo kwa mitihani ya ujirani mwema.

Hali ilizidi kuwa mbaya zaidi kwa wazazi wa wanafunzi waliokufa katika ajali hiyo kwani hawakuweza kujizuia na kila mmoja aliangua kilio pale alipoona jeneza la mtoto wake likiwa na msalaba na kuandikwa jina kamili. Hali hiyo ya kilio kwa kila mzazi ilisababisha hata viongozi mbalimbali wa serikali na vyama wakiongozwa na Makamu wa Rais, Samia waliokuwepo katika ibada hiyo maalumu, kuinamisha vichwa vyao kwa simanzi na wengine kujikaza kwa kufuta machozi kwa vitambaa vyao vya mikononi.

MAKAMU WA RAIS Akizungumza katika ibada hiyo maalumu, Makamu wa Rais, Samia amewataka madereva kote nchini kuwa waangalifu na makini wanapofanya kazi zao za kila siku kwani wajue kuwa wanabeba roho za watu. Alisema serikali kila siku imekuwa ikiwakumbusha madereva kuacha kutumia vilevi pindi wanapoendesha vyombo vya moto kwani kwa kufanya hivyo ni kutenda kosa kubwa sana, na aliwakumbusha madereva kuwa iwapo watakuwa makini na waangalifu katika kuendesha magari, ajali nyingi zinaweza kuepukika.

Mbali ya hilo, amewataka wamiliki wa magari na madereva kubeba abiria wanaostahili katika vyombo vyao vya usafiri kwa kufanya hivyo kunaweza kuepuka ajali. Alisema vifo vya wanafunzi, walimu na dereva wa shule hiyo ya awali na msingi yenye makao yake Kwamrombo jijini hapa, vimeleta huzuni kubwa sana kwa nchi na Rais John Magufuli ametoa salamu za kuwapa pole sana wafiwa na wakazi wote wa Jiji la Arusha kutokana na msiba huo mkubwa. Aliwashukuru watalii ambao ni madaktari bingwa kutoka Marekani kwa msaada mkubwa waliotoa ajali ilipotokea na kuwataka kuendeleza ukarimu huo sehemu yoyote bila ya kificho.

Alisema madaktari hao baada ya ajali ndio waliokuwa wa kwanza kufika katika eneo la tukio na kutoa huduma ya kwanza na hatimaye kufuatilia hadi hospitalini walikopelekwa, hiyo ni kiasi gani walitimiza wajibu wao wa upendo kwa nchi kwa kuwashughulikia majeruhi na wengine kupoteza masiha. Makamu wa Rais alimshukuru Rais Uhuru Kenyatta na wananchi wake wa Kenya kwa kushiriki kikamilifu katika msiba huo na pia kumtuma Waziri wa Elimu kushiriki ibada hiyo inatia moyo ni jinsi gani Kenya ilivyo karibu na Tanzania.

MBOWE Naye Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, alisema jana ilikuwa siku muhimu sana kila Mtanzania kutafakari amani ya kitaifa. Mbowe alisema Chadema na vyama vyote vya upinzani vitakuwa mstari wa mbele na Serikali Kuu na Mkoa katika kuhakikisha kila jambo la msingi linakwenda sawa na kuwapa pole wale wote waliofikwa na msiba huo.

Alisema msiba huu ni mkubwa na Watanzania wote. KINANA Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, kwa niaba ya wanachama wa chama hicho kote nchini na wabunge wake, alitoa pole nyingi sana kwa msiba huo na kuwataka wafiwa kuwa na uvumilivu katika kipindi hicho kigumu kwao. Kinana aliyeingia uwanjani hapo na Makamu wa Rais saa 3.40 asubuhi, alisema kila mtu aliyekuja uwanjani hapo ana dini na kifo ndicho huunganisha watu na kuacha tofauti zao na kuangalia kilicho mbele.

Alitumia muda mfupi sana kuongea na kuwataka wakazi wa Jiji la Arusha, wazazi na walimu kuwa wapole katika wakati huu. WAZIRI WA ELIMU KENYA Kabla ya kuingia kwa miili hiyo uwanjani, kulikuwa na salamu za viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Elimu wa Kenya, Fred Matiang’i, ambaye alisema ametumwa na Rais Uhuru, kuwa nchi yake imeguswa na msiba huo mkubwa. Matiang’i alisema wananchi wa Kenya wakiongozwa na Rais wao, wako bega kwa bega na Serikali ya Tanzania katika kuomboleza msiba huo na kuwapa pole wazazi, walezi na ndugu wa wanafunzi, walimu na dereva waliokufa katika ajali hiyo.

“Nimekuja hapa siku ya leo nimetumwa na Rais Uhuru kutoa pole na rambirambi za vifo hivyo na Kenya nzima imehuzunishwa sana, na Serikali ya Kenya imetoa pole sana kwa wale wote waliofiwa. Mungu aendelee kuwafariji na kuwapa pole katika kipindi hiki kigumu kwani sisi sote ni wamoja na katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na ni lazima tushirikiane kwa hali na mali katika kila jambo,” alieleza waziri huyo wa Elimu Kenya.

SALAMU ZA SMZ Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed, alisema kwa niaba ya Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Serikali ya Baraza la Mapinduzi wamesikitishwa na tukio hilo na wako katika majonzi na huzuni kubwa kwa msiba huo. Aboud alisema SMZ iko mstari wa mbele katika jambo hilo na kuwataka wazazi, walezi na ndugu kuwapa pole katika kipindi hiki kigumu na wao watatoa rambirambi ikiwa ni njia ya kuwafariji wafiwa.

MAWAZIRI WATOA NENO Vingozi wengine waliopata fursa ya kuzungumza ni baadhi ya mawaziri, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.

Pia walikuwapo viongozi wa dini, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa. Dk Mpango alisema alikuwa Arusha kushiriki kikao cha bajeti na mawaziri wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), lakini alipopata taarifa hiyo ilimsikitisha na hakutaka kuondoka na kusubiri ibada jana. Alisema watoto na wengine waliofariki katika ajali hiyo wanapaswa kupongezwa kwani wamefariki wakiwa kazini wakisaka elimu. Kwa upande wake, Profesa Ndalichako alisema wanafunzi na walimu wamekufa wakiwa katika harakati za kusaka elimu hivyo kazi ya Mungu haina makosa.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera, alisema kwa niaba ya wakuu wa mikoa yote na yeye kama jirani anawapa pole sana wazazi na wananchi wote wa Arusha. Bendera alisema msiba hauzoeleki na kila mtu ameguswa na msiba huo na kila mmoja wetu anawapenda sana wanafunzi na walimu wao, lakini Mungu amewapenda sana na ndio maana amewachukua ghafla.

KAIMU JAJII MKUU Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, aliwapa pole wale wote waliofiwa na kusema hiyo ilikuwa mipango ya Mungu. Jaji Juma alisema binadamu hupanga mipango yake, lakini Mungu naye hupanga mipango na kutekeleza na kuwataka wafiwa kuwa wapole katika kipindi hiki kigumu kwao. Alisema watoto hao walikuwa wakisaka mwanga wa elimu hivyo wanapaswa kuombewa kule waendako wapate mwanga zaidi.

MAENEO WANAKOZIKWA Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Gambo, wanafunzi waliopata ajali ya kufa wanasafirishwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwamo ya Nyanda za Juu Kusini katika Mkoa wa Iringa, Kyela mkoani Mbeya na Mkoa wa Tanga. Gambo alitaja maeneo mengine ya mbali ambayo yamegharamiwa na serikali ni mkoani Singida, Kondoa mkoani Dodoma, Rombo Mkoani Kilimanjaro na wanafunzi wengine wanazikwa jijini Arusha katika maeneo ambayo wafiwa watakuwa tayari kusema .

Pia baadhi ya miili ya watoto kadhaa imerudishwa hospitali walimokuwa wamepumzishwa wakisubiri siku ya kuzikwa jijini hapa; wengine wanazikwa leo, wengine kesho hadi Ijumaa katika maeneo tofauti. Gambo alisema gharama za majeneza, usafiri na nyingine zote zinagharamiwa na Serikali ya Mkoa wa Arusha na kuwataka wafiwa kushirikiana na kamati kwa kila jambo. SHULE YAFUNGWA Kwa mujibu wa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Lucky Vincent, Ephraim Jackson, shule hiyo imefungwa kwa wiki moja kwa sababu ya maombolezo ya msiba huo.

Nipe maoni yako kwa kubonyeza

===== NAZIRHAMZA

Operation yaendelea Rwanda kuhusiana na mauaji ya kimbali

WATUHUMIWA nane vinara wa mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda mwaka 1994, bado wanasakwa kwa udi na uvumba na Umoja wa Mataifa ili wajibu tuhuma za ushiriki wao katika mauaji ya watu milioni moja nchini humo wengi wao wakiwa Watutsi.

Kati ya hao nane, watatu ambao ndio watuhumiwa wakuu watashtakiwa katika chombo kinachosimamia kazi zilizobaki za iliyokuwa Mahakama ya Mauaji Kimbari ya Rwanda (ICTR) ambayo imemaliza muda wake miaka miwili iliyopita.

Chombo hicho (MICT) kimepewa majukumu ya kuwatafuta, kuwakamata na kuwashtaki watuhumiwa watatu vinara wa mauaji hayo wakiongozwa na mfanyabiashara Felicien Kabuga ambaye anatajwa kuwa mmoja wa vinara wa mauaji hayo ya siku 100 nchini humo.

Ofisa Habari wa MICT,Danford Mpumillwa alisema mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa kazi ya kuwasaka watuhumiwa hao inaendelea kwa kushirikiana na serikali za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Aliwataja watuhumiwa wengine wawili vinara ambao wakikamatwa watafikishwa katika MICT mjini  Arusha kuwa ni Augustin Bizimana ambaye alikuwa Waziri wa Ulinzi katika serikali ya Rais Juvenal Habyarimana na Protais Mpiranya  aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha kumlinda Rais Habyerimana.

Watuhumiwa wengine watano, kwa mujibu wa Mpumillwa, wakikamatwa watapelekwa Rwanda kushtakiwa ambao ni Fulgence Kayishema, Charles Sikubwabo, Aloys Ndimbati, Pheneas Munyarugarama na mwingine aliyefahamika kwa jina moja tu la Ryandikayo.

“Nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa zinawajibika kuwakamata na kuwafikisha katika chombo hicho watuhumiwa hao na kikosi maalum cha kuwasaka kinaendelea kuwafuatilia katika nchi ambazo tunaamini wamejificha. Sasa ni wajibu wa serikali husika kushirikiana kuwakamata watuhumiwa ili wakajibu tuhuma dhidi yao na hii ni kazi ya kudumu,” alisisitiza Mpumillwa wakati wa mkutano wa pamoja wa majaji wa Chombo hicho, Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu (ACPHR), Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) na Mahakama Kuu ya Tanzania.

Akizungumza baada ya ufunguzi wa mkutano huo wa pili kufanyika Afrika, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma alisema kuwa una lenga kubadilishana uzoefu katika utoaji wa haki nchini.

“Tunajifunza kutoka kwa wenzetu namna bora na mazingira yatakayosaidia utoaji wa haki hapa nchini kwa kuzingatia uzoefu wa wenzetu na uwezo wa rasilimali walizonazo na hii itasaidia nasi kuiga yale yaliyo ndani ya uwezo wetu,” alisisitiza Profesa Juma.

 MICT ni chombo kilichoundwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa baada ya ICTR kumaliza muda wake kusimamia kesi zilizobaki na kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka muhimu za kesi hizo zitakazotumiwa na wasomi kwa ajili ya utafiti wa kitaaluma kikiwa na makao makuu yake Lakilaki eneo la Kisongo jijini hapa.
Au maoni yako Kupitia
NazirHamza au

FacebookTwitterGoogle+WhatsAppPinterestShare

Jumatatu, Mei 08, 2017

Ajali mbaya yaiyumbishi kwa ujumla


SIKU ya Mei 6 mwaka huu (2017) ni kati siku zitakazokumbukwa na wakazi Arusha na Tanzania kwa ujumla wake kwa muda mrefu.

Siku hii imeacha kumbukumbu mbaya kufuatia ajali mbaya ya gari iliyopoteza uhai wa wanafunzi 33 wa shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Lucky Vicent iliyopo eneo la Kwa Mrombo katika Jiji  la Arusha.

Pamoja na wanafunzi hao 33 ambao wote ni wa darasa la saba pia katika ajali hiyo maisha ya walimu wawili wa shule hiyo, Innocent Pappian na Julius Mollel na dereva Dismas Kessy, walipoteza maisha hivyo kufanya idadi ya waliofariki katika ajali kufikia watu 36.

Walionusurika katika ajali hiyo ni wanafunzi wawili wa kike ambao hadi usiku wa kuamkia leo (Mei 7, 2017) walikuwa wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru ambao hata hivyo majina yao hayakuweza kupatikana mara moja.

Ajali hiyo mbaya ambayo itabaki katika kumbukumbu za ajali mbaya kuwahi kutokea mkoani Arusha na nchini ilitokea saa 2.30 asubuhi (Mei 6) katika kijiji cha Rhotia baada ya gari hilo kuacha barabara na kutumbukia katika korongo la mto Marera, lenye urefu unaokadiriwa kuwa kati ya mita 20 hadi 25.

Wanafunzi hao waliokuwa wakitumia usafiri wa basi la shule aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili  T 872 BYS  walikuwa safarini kuelekea wilayani Karatu, kushiriki mitihani ya ujirani mwema na wenzao wa shule ya Tumaini Academy iliyopo mjini Karatu.

Basi hilo lilikuwa kati ya mabasi matatu ya shule hiyo yaliyokuwa yameongozana na taarifa  kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa gari iliyopata ajali ilikuwa katikati.

Taarifa kutoka eneo la tukio na chanzo cha ajali

Bado hakuna uhakika wa taarifa rasmi kuhusu chanzo cha ajali hiyo lakini taarifa zilizopo zinadai kuwa ni kutokana na mfumo wa breki za gari hilo kushindwa kufanya kazi na hivyo dereva kushindwa kumudu usukani na gari kutumbukia korongoni.

Aidha taarifa nyingine zinadai kuwa dereva huyo alikuwa katika mwendo kasi eneo hilo ambalo lina mteremko mkali na kona kali  hivyo kushindwa kuhimili mwendo kasi wa gari lake.

Lakini Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo aliwaambia waandishi wa habari kwamba polisi bado wanachungunza chanzo cha ajali hiyo na taarifa itatolewa kwa umma uchunguzi huo utakapokamilika.

Taarifa zilizopatika kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa wanafunzi 29 walifariki papo hapo pamoja na walimu wao wawili na dereva wa gari hilo na kufanya idadi ya waliokufa wakati huo kuwa 32.

Majeruhi walikimbizwa katika hospitali teule ya Wilaya Karatu na kituo cha afya cha Rhotia  ambapo inaelezwa kuwa watatu walifariki dunia wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali teule na majeruhi watatu walihamishiwa Hospitali ya Mkoa wa Arusha ambapo mmoja alifariki dunia saa 10 jioni hivyo kubakia wawili ambao wote ni wasichana.

Habari kutoka kwa mashuhuda wa ajali zinadai kuwa polisi wakishirikiana na wananchi wa kijiji hicho pamoja na wapita njia walianza uokoaji mara moja baada ya kutokea kwa ajali.

Kutokana na kuharibika vibaya kwa gari hilo wananchi  hao walitumia mashoka, mitarimbo, nyundo, majembe na vifaa vingine kutoa miili ya marehemu na majeruhi.

“Hali ilikuwa ya kutisha na kuogofya katika eneo la ajali, miili mingi iliyotolewa ilikuwa na majeraha makubwa ya kutisha na wengi walikuwa wamevunjika viungo vyao,” alidai mmoja kati ya waokoaji ambaye hakutaka kutajwa gazetini.

Majonzi, vilio, Mount Meru Hospitali

Hali ilikuwa ya kusikitisha katika Hospitali ya Mount Meru ambapo vilio, majonzi, simanzi vilitanda kila kona na kila mmoja  wakiwamo madaktari, wauguzi, viongozi wa serikali na wa kisiasa walionekana kuguswa na tukio hilo.

Umati mkubwa wa wakazi wa Arusha na vitongoji vyake  ulianza kukusanyika kuanzia saa 6 mchana baada ya taarifa kuzagaa kuwa majeruhi pamoja na miili ya waliofariki ilikuwa njia kuletwa hospitalini hapo.

Hadi kufikia saa 9 alasiri eneo lote la hospitali lilikuwa limefurika watu na barabara maarufu ya Afrika Mashariki nayo ilikuwa imefurika kiasi kwamba magari yalilazimika kupita kwa taabu.

Aidha eneo la kuhifadhia chumba cha maiti nalo lilikuwa limefurika watu ambao walikuwa wakisubiri kuona na kutambua miili ya wapendwa wao hali iliyowalazimu polisi wa kikosi cha FFU waliokuwa na silaha nzito kuimarisha ulinzi.

Ilipotimu saa 9.46 alasiri miili ya majeruhi watatu iliwasili kwa magari ya kubeba wagonjwa (ambulance) na ndipo viliposikika vilio kutoka kila kona ya viwanja vya hospitali hiyo.

Baadaye umati huo ulihamia katika eneo la chumba cha kuhifadhia maiti na miili ilipowasili polisi walishindwa kuthibiti hali kutokana na wazazi na ndugu wa marehemu kushinikiza kuwa wanataka kutambua miili ya watoto wao.

Kutokana na hali hiyo, ilimlazimu Mkuu wa Wilaya Arusha, Gabriel Dagharo, kuingilia kati na kuwataka wale tu waliofiwa waruhusiwe kuingia ndani ya chumba cha maiti kutambua miili ya watoto wao.

Kauli za viongozi

Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Dagharro, alisema binafsi na serikali amesikitishwa na msiba huo na kuongeza kuwa, serikali iko pamoja na wazazi walipoteza watoto wao.

“Msiba huu umetugusa wote, si msiba wa watu wa Arusha peke yao huu ni msiba wa taifa na ndiyo maana Rais wetu ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha na watu wote wa Arusha,” alisema.

Alisema wakati viongozi wa serikali wakikutana kufanya taratibu za mazishi kwa kusaidiana na familia ibada ya pamoja ya kuaga miili itafanyika katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid siku ya Jumatatu kuanzia saa 6 za mchana.

Kwa upande wake Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro, alisema anaungana na wazazi na wanafamilia katika kipindi hiki kigumu cha kupotea kwa maisha ya wanafunzi hao na walimu wao.

“Hakuna jambo limetuumiza watu wa Arusha kama ajali hii, natoa pole kwa wazazi na wamiliki wa shule. Naomba tuungane sote bila kujali itikadi zetu za kisiasa na imani zetu za dini huu msiba ni wetu sote watu wa Arusha na Watanzania kwa ujumla,” alisema.

Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Longino Vicent Nkana, aliwaambia waandishi wa habari kuwa wanafunzi hao waliondoka shuleni hapo saa 12.30 asubuhi  kuelekea Karatu kwa ajili ya kushiriki mitihani hiyo ya ujirani mwema.

Alieleza kuwa wamekuwa wakifanya mitihani hiyo ya ujirani mwema kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa zaidi ya miaka mitatu sasa na hakukuwahi kutokea tatizo lolote.

“Magari yetu hufanyiwa matengenezo katika karakana zetu mbili kila wiki na yako salama na hata wakati mwingine tunakodishwa kwa shughuli nyingine za kijamii,” alifafanua.

Aliongeza kuwa shule hiyo ilianzishwa mwaka 2006 na imekuwa katika shule bora kitaaluma mkoani Arusha ambapo mwaka 2016 ilishika nafasi ya pili ngazi ya mkoa katika mitihani ya darasa la saba.

MOMOGORO BLOG: IMEBAHATIKA KUPATA MAJINA MACHACHE YA WATOTO WALIOPOTEZA MAISHA HUKO ARUSHA

Majina ya waliofariki yaliyopatikana ni pamoja na Mteage Amos, Justine Alex, Irene Kishari, Gladness Goodluck, Praise Roland, Shadrack Biketh, Junior Mwashuye, Aisha Said, Oumligh Herri Rashid, Gema Gerald, Rebecca Daudi, Hagai Lucas, Said Ally na Ruth Ndemna.

Wengine ni Atusa Kassim, Neema Eliwashi, Neema Martine, Greyson Robson Masana, Heavennight  Enock, Ian Tarimo Anold Alex, Naomia Hosea, Rukia Altam, Eliapendo Elihudi, Marion Mrema, Rehema Msuya, Sabrina Said na Prisca Charles.

Majina mengine zaidi yanatarajiwa kutolewa hapo baadaye leo.

Nitumie maoni yako Kupitia Facebook.com/proffesa nazir
Au
Nicheki == NAZIRHAMZA

Askofu afunguliwa mashtaka baada ya kuoa Mke wa Mu umini wake

Karagwe. Mchungaji wa kanisa la huduma katika roho wilayani Karagwe, Jafece Josephat anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani humo baada ya kumuoa mke wa muumini wake na kuanza kuishi naye kama mke na mume akidai ameoteshwa na Mungu.
Mchungaji huyo amekamatwa leo baada ya kamati ya ulinzi na usalama na kamati ya amani na maadili ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo, Godfrey Mheruka kufika kanisani hapo na kupata ukweli juu ya jambo hilo baada ya pande zote akiwemo mchungaji wa kanisa Josephat, mwanamke aliyefahamika kwa jina la Domina Damian na mme wake wa mwanzo Donath Appolo kueleza ukweli jinsi walivyooteshwa mpaka hatua ya mke kuolewa.
Mheruka alitoa agizo la kukamatwa kwa mchungaji huyo kutokana na baba wa Appolo aliyenyanganywa mke kujitokeza mbele ya kanisa hilo na kudai mahari aliyomtolea mtoto wake irudishwe kwani hawezi kuutolea mahari ukoo mwingine kwa kuwa mke ameshaolewa na mme mwingine.
"Kwa kuwa, mke ameacha familia yake akaja kuolewa na wewe mchungaji amezini na kwa kuwa wewe unayejiita mchungaji umeiacha familia yako ya watoto watano ukaoa mke mwingine nyote mnazini kwani kinachotenganisha ndoa ya mke na mme ni kifo lakini nyie mmejichukulia maamuzi yenu binafsi,"amesema Mheruka.
Mheruka amemwagiza mwangalizi wa kanisa hilo kuendelea kutoa huduma katika kanisa hilo ndani ya miezi sita huku akitafuta utaratibu wa mchungaji mwingine mwenye maadili mema na kuwa wao kama Serikali watachunguza vizuri kama kanisa hilo limesajiliwa au halijasajiliwa ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa.

Nitumie maoni yako Kupitia Facebook.com/proffesa%nazirhamzatz